Mchezo wa Kukata Kiuno

quinta-feira, 15 de março de 2012

Ni kweli wanaume wanapenda wanawake wenye matiti makubwa?

JIBU ni ndiyo kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Uingereza kisha kuripotiwa na Jarida la New Study umebainisha kwamba, wanawake wenye matiti makubwa huwasisimua zaidi wanaume kimapenzi kuliko wengine.
Jane Pincott Mwandishi wa masuala ya sayansi amekiri katika kitabu chake cha ‘Do Gentleman Really Prefer Brondes’ kwa kueleza kinagaubaga juu ya utafiti huo kuwa, nguvu ya mvuto wa wanawake wa aina hiyo ni kubwa na kufafanua kwamba ina uwezo maradufu wa kuteka hisia za wanaume.
“Hakuna mwenye kupinga kuhusu hili, dunia nzima inafahamu na hasa wanaume wenyewe…kigezo cha kwanza cha kumtambua mwanamke ni matiti, …kadri yanavyokuwa makubwa utambulisho wake hukua na mvuto huongezeka.
“Mwanamke kuwa na sura nzuri peke yake haitoshi…ingawa wanaume hupenda hilo pia, lakini si jambo linaloamsha hisia zao za mapenzi haraka, tumetafiti na kubaini ukweli huu tunaoueleza,” alisema Pincott alipozungumza na jarida hilo la New Study.
Timu ya wataalamu iliyoendesha utafiti huo, ilihusisha zaidi ya wanaume 4,000,kwa kuwaweka kwenye chumba chenye picha za wanawake wenye matiti makubwa na madogo, ambapo ilibainika asilimia 79 ya waliotazama picha za wanawake wenye matiti makubwa walisisimka kimapenzi.
Naye Dk. Grazyna Jasienska wa Chuo cha Harvard aliongezea nyama kwenye uchunguzi huo kwa kusema kuwa, mwanamke mwenye matiti makubwa ana uwezo wa kushika ujauzito haraka kuliko n mwenye matati madogo.
Ripoti hiyo ya watafiti wa nje inaweza kuwa na ukweli hata kwa wanawake wa kibongo ambao nyakati hizi wamekuwa wakiacha nje sehemu kubwa ya matiti yao makubwa, bila kubainisha sababu hasa za kufanya hivyo.
Mimi nakubaliana kwa kiasi fulani na utafiti huo kwa sababu za kitaalamu, matiti ni kiungo nyeti chenye hisia za mapenzi, kinapoonekana kwa wazi huvutia, hii haijalishi kama matiti ni makubwa au madogo.
Lakini kwa kuwa matiti makubwa huonekana kirahisi mwanamke anapokuwa amevaa nguo, hiyo inaweza kuwa sababu ya wenye matiti hayo kuvutia, hili halina ubishi.
Lakini pamoja na uweli huo bado suala hili linabaki kwenye mtazamo wa kila mwanaume, kwani wapo wanaopenda wanawake wenye matiti madogo, lakini kama nilivyosema kuonekana kwa matiti hayo kunabaki kuwa ni jambo pekee linaloweza kuamsha hisia za mwanaume.
Hii ina maana kwamba hata kama mwanamke atakuwa na matiti madogo na akayaweka wazi atakuwa amefanya kile kile kinachoweza kufanywa na mwenye matiti makubwa.

Sem comentários:

Publicar um comentário