Mchezo wa Kukata Kiuno

quinta-feira, 20 de dezembro de 2012

Jamaa huyu apata tigo


sábado, 17 de março de 2012

Ukitaka furaha, gharamia kwanza furaha ya mwenzi wako

SANAA ya busara katika maisha inajumuisha vitu vinne: Nia na malengo, Mungu ana nafasi yake, hatua chanya na mafanikio endelevu. Ukikaribisha busara kama kanuni yako ya kuishi, maana yake unahitaji amani na furaha.

Ukitaka kuishi kwa busara ni lazima uwe na mtazamo wenye furaha. Lazima uingalie dunia kwa fikra na macho, angalia jinsi watu wengine wanavyosononeka kwa kuikosa, halafu chukua mfano wa wanaoshi kwa amani yenye afya.

Unapoitazama dunia kwa fikra, hapo unapaswa kubeba ufahamu wa uchafu mgumu uliopo. Fikra zinakuja kutokana na kumbukumbu ambazo hutafsiri uzoefu wa nyuma ambao utakupa mwanga wa hali ya sasa. Hatua hizo zinatakiwa kutoa muongozo katika kuandaa furaha.

Mwandishi wa saikolojia, Swami Sukhabodhanda katika makala yake yenye kichwa “Love and Happiness: Art of Wise Living Brings Great Joy” ameandika:

“Mtu sahihi ni yule anayejifunza kupunguza msongo wa mawazo, Anayejifunza kuongeza furaha na kupanua uwezo wake.”
Hii ina maana kuwa kutafuta furaha ni wajibu wako, lakini swali la kujiuliza ni hili, mwenzi wako akiwa hana amani wewe utaipata wapi? Akiwa amekasirika utaweza kucheka? Jibu ni kwamba haiwezekani na endapo moyo wako una amani wakati mwenzako amejikunja, ni wazi kwamba penzi lenu limejaa mashaka.

Hivyo basi, naungana na Swami kushauri kwamba ni lazima kila mtu ajifunze kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza furaha. Ukifanikiwa kuiweka chanya furaha ya mwenzi wako na yako itapatikana. Zingatia msemo kuwa ninyi ni kitu kimoja wewe ni yeye!

Watu wengi wamekuwa wakishindwa kustawisha uhusiano wao kwa sababu wanashindwa kuishi ndani ya wenzao. Wanatenda mambo ambayo yanawaumiza wenzi wao bila kujiuliza. Hawana malengo chanya!

Mtu mwenye malengo mazuri katika mapenzi ni yule ambaye anajiuliza kabla ya kuzungumza au kutenda. Anatafakari kauli au kitendo na matokeo yake. Pointi kuu ni mapokeo ya mwenzi wake. Ni kosa kufanya tukio lolote au kutoa matamshi yanayoweza kumuudhi mwenzako.

Ni lazima uwe na angalizo kwamba kwako linaweza kuwa dogo lakini kwa mwenzako ni kubwa. Heshimu kosa lolote kwamba linaweza kuhatarisha uhusiano wako, kwa hiyo jichunge kila eneo.

Wewe ni mtu tu duniani, inawezekana uzito wako ni mdogo. Ukiwepo na usiwepo taifa halisomi upungufu wowote! Hata hivyo, kupitia mapenzi wewe ni dunia mbele ya mwenzi wako. Kila kitu hakina thamani kwake bila uwepo wake, kwa hiyo heshimu hisia zake, ingia gharama kumletea furaha.

Nimeeleza hapo juu kuwa mfumo sahihi wa mapenzi ni kuishi ndani ya mwenzake. Yaani kuzijulia hisia zake na kujenga nidhamu ya kuepuka kumpa maumivu yasiyo na sababu. Unaelewa kuwa mwenzako hapendi uchelewe kurudi nyumbani, kwa hiyo usifanye makusudi kuchelewa mitaani.

Ni kweli unapenda kuketi na wafanyakazi wenzako au marafiki mkipata za moto na baridi baada ya kazi. Lakini wakati unatekeleza hilo, kwa kila hatua jiulize, je, hicho ndicho ambacho mwenzi wako anakihitaji? Kama ndiyo basi fanya, ikiwa jibu ni kinyume chake, changamsha miguu umuwahi nyumbani.

Jiulize swali; Kuna sababu gani ya kugandana na marafiki mitaani wakati mwenzako amenuna nyumbani? Jiongeze lingine; Mtakapokuwa ‘mnaparurana’ nyumbani hao unaowaendekeza watakuwepo? Pengine wakati wao wanalala usingizi mzuri, wewe kwako hakulaliki.

Tafakari; Kuna mambo mengi ambayo mnachangia pamoja, ulimwengu ambao unapita naye ni usiku wa giza kwa wengine. Hulioni kama hilo ni maalum? Tambua thamani ya mwenzi wako, hivyo tekeleza furaha yake na umtimizie kwa vipimo sahihi.

Furaha ya mpenzi wako ni gharama, kwa hiyo unahitaji kujipanga ili kumtimizia. Katika uhusiano wa kimapenzi, hauna cha kupoteza kwa kugharamia amani na furaha ya mpenzi wako. Umegundua kwamba ili mwenzio awe sawa ni lazima uende Zanzibar, uwezo upo fanya hivyo!

Tafsiri yake ni kuwa unatakiwa kufanya kila linalowezekana ili mpenzi wako awe na furaha. Sifa ya ubabe na kupuuza hisia za mwenzi wako haina maana. Ukimpuuza leo, maana yake unataka kesho akupuuze. Akikutenda wewe utafurahi? Usingoje msemo wa mkuki kwa nguruwe ukufike!

Zipo hasara nyingi ambazo unaweza kukutana nazo endapo utashindwa kugharamia furaha ya mwenzi wako. Hii inamaana kuwa ni vema unisome vizuri ili ujifunze.

Asilimia kubwa ya watu ambao wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, husumbuliwa na tatizo la kutotengeneza penzi. Wakiongozwa na msemo kuwa kila kitu hupangwa na Mungu, nao huacha mapenzi yao yaende kama yalivyo. Hawaamini kuwa barabara ilichongwa, ndiyo magari yakapita.

Ukiona vyaelea ujue vimeundwa! Hii inamaana kuwa kila kinachostawi, nyuma yake kuna ujenzi uliofanyika. Usimuone babu na bibi wanasherehekea miaka 50 ya ndoa yao ukadhani ni jambo lililokuja lenyewe. Kuna mambo ya msingi ambayo waliyafanya kuhakikisha wanadumu mpaka kuzikana.

Ukiwa mwingi wa hasira, matatizo yanayotokea hutaki kuyaweka mezani ili myajadili na kuyamaliza, kila siku utakuwa unabadili uhusiano. La! Hutabadili lakini utabaki kwenye penzi ambalo unaishi bila amani. Huna furaha! Ni mpenzi lakini hamfungamani, mnakuwa kama wapinzani wa jadi!

Uhusiano bora ni ule ambao wanaoujenga ni watu makini na ambao wanajua nini ambacho wanakifanya. Wenye kufahamu thamani ya penzi lao kila mmoja anaheshimu umuhimu wa mwenzake. Wanaoguswa kutoa chochote kuhakikisha wanaendelea kuwa bora kimapenzi.

Hii ndiyo sababu ya kukutaka uhangaike na ikiwezekana utumie gharama yoyote ili mwenzi wako awe na furaha. Utengeneze thamani yako kwake, kiasi kwamba akikuona aone mbele yake kasimama mtu aliyeishikilia dunia yake. Inawezekana! Mapenzi ni ujanja, utundu, kuguswa na kujitolea!

Huna sababu ya kushindwa kugharamia furaha ya mwenzi wako kwa sababu ukiacha gharama yake ni kubwa. Utakosa kila kitu muhimu ambacho mtu sahihi angependa kupata kutoka kwa mwenzi wake. Na hiyo itakusumbua! Kama hutafikiria, basi utaona kwa wengine na utatamani!

Hapa chini nakuchambulia hasara ambazo unaweza kukutana nazo kwa kushindwa kuhudumia furaha ya mwenzi wako;

UTAKOSA AMANI
Misongo (stresses) ya kimaisha inatesa. Inawezekana unafanya kazi sana. Wakati mwingine masuala ya kiofisi au biashara hayaendi kama inavyotakiwa. Unashinda siku nzima ukipigana kuhakikisha unaendelea mbele. Iwe umeajiriwa, umejiajiri au umeajiri! Kichwa hakitulii mpaka unahisi ni kizito.

Kufikia hapo, bila shaka unahitaji faraja. Ni kipindi ambacho huhitaji mwenzi sahihi ili aweze kukusahaulisha matatizo ya kimaisha. Mtu ambaye anakujua ulivyo, kwa hiyo inamuwia rahisi kutambua kwamba upo kwenye matatizo na kuchukua hatua zinazofaa kurekebisha hali.

Fikiria kwamba ukiwa katika hali hiyo, unarudi nyumbani ambako unakutana na moto mwingine. Amani hakuna! Kichwa chako kinaweza kuchanganyikiwa. Kama sivyo, maradhi ya moyo yatakunyemelea. Kupata kilicho bora, kiandae. Lima shamba na kupalilia ili upate mavuno mazuri.

Ukifanikiwa kumuweka mwenzi wako katika hali ya furaha, utapata faraja muda wote. Yakikufika, ukirejea nyumbani utakuta amani. Utakutana na tiba ya msongo wa mawazo ulionao. Hiyo ndiyo tafsiri ya upendo, kwa hiyo usije kukosa utulivu wa moyo. Anza leo kumfurahisha ili naye akupe mahaba tele!

UTACHOKWA HARAKA
Hakuna kitu kibaya kwenye mapenzi kama mtu kuchokwa na mwenzi wake. Lakini hilo siyo zito, ni rahisi mno kama hutoamua kushughulikia kasoro ulizonazo.

Huna ubunifu, mwenzi wako haoni kitu chochote kipya. Mwenzi wako hana furaha wewe hujishughulishi. Ataanza kukuona ni mzigo na mwisho atakuchoka. Usikubali hali hiyo ikutokee, anza leo! Maisha ya kimapenzi ni mazuri sana endapo utaamua.

MTASHINDWA KUJADILIANA
Mwenzi wako hana furaha, wewe unaingia mlango huu naye anapitia ule. Hayo ni maisha mabaya mno! Mnapatwa na mambo ambayo mngependa kushauriana, lakini mnashindwa kufanya hivyo kwa sababu mnaishi kama Simba na Yanga.

Kuna watu wanaishi kwa kalamu, wanalala mzungu wa nne! Kama matumizi, yanawekwa mezani, akitaka kutoa agizo anaandika ‘kimemo’ na kukiacha juu ya stuli! Hawaguswi kutafuta furaha yao, hawataki kuzungumza na kumaliza tofauti zao.

Matokeo yake ni siri za ndani kuzagaa mitaani. Hili likikufika ni sawa na msiba. Chukua hatua!

HUTAPATA HUDUMA BORA
Mwenzi wako anahitaji kuwa na furaha ili aweze kukupa huduma bora. Amini kwamba mwenzi wako ndiye ambaye anaweza kukufanya hii dunia uione yote ni yako. Changamka leo!

Unahitaji huduma bora kutoka kwa mwenzi wako, na hilo anaweza kulitimiza endapo atakuwa na furaha dhidi yako. Hii inamaana kwamba kuanzia sasa, punguza maudhi kwa mwenzi wako na umzidishie amani. Akupende na aamini ndani ya nafsi yake kwamba wewe ndiye mtu bora zaidi maishani mwake.

Ukimfurahisha, atakupa huduma bora ambayo huwezi kuipata popote. Bila shaka atakapokuhudumia, nawe utajiona umepata mwenzi sahihi wa maisha yako. Hayo ndiyo mapenzi. Yakistawishwa hustawi!

Ukijichanganya kwenye mapenzi, utapoteza mwelekeo wa maisha

Unaweza kuona ni kama swali la kipuuzi lakini lazima lipate jibu. Katika uchunguzi wangu kuna kitu ambacho nimekigundua, katika mapenzi ya sasa hivi eti wanajiita kwenda na wakati (dot com). Kumekuwa na tabia ya kukosekana kwa uaminifu, watu wamekuwa wakizungukana, hata marafiki.

Hii imekuwa ikiwakuta wasichana wengi hasa wanafunzi ambao wamekuwa wakiingia katika mapenzi bila kujua nini hasa maana ya mapenzi. Wengi wao huona kuwa na mpenzi ni fasheni, kumbe mapenzi ni maisha kamili, ambayo kama utafanya vibaya huenda ukavuruka mpangilio wako wote wa maisha yako.

Nia yangu kubwa si kuwagusa wanafunzi ambao wamekuwa ndiyo wanaongoza kwa kuuliza maswali juu ya penzi lao kukosa muelekeo. Naomba twende pamoja ili tujue njia ya mapenzi ni ipi ambayo siku zote itakufanya uwe na penzi salama.


Siku zote unapoanza mapenzi hakikisha yule unayetaka kumkabidhi dhamana ya moyo na mwili wako yupo vipi. Usikurupuke kwa vile umeambiwa unapendwa, kuutoa mwili wako kwa mtu si jambo la mzaha hata kidogo.

Chukua muda wako kupata undani wa mtu anayetaka kuuhifadhi moyo wako, kwani kosa lako linaweza kukutia kwenye mateso makubwa. Japo kumjua mpenzi wa kweli yahitaji kutumia muda mrefu, lakini ni vizuri kuvuta subra kabla hujatoa uamuzi.

Pia unapokuwa umeanzisha uhusiano jiepushe kuchanganya wapenzi, anaweza kutokea mtu ambaye hakika moyo wake ulikuwa radhi kufanya lolote hata kuachika kwa ajili yako. Lakini bahati mbaya umo ndani ya ndoa au ndani ya penzi miliki.

Mapenzi yana njia moja, penzi la kweli ni lile ulilomo na wala si la pembeni. Sawa na mashindano ya riadha ya mita 100, ukikimbia katika mstari wa mwenzako utakuwa umefanya makosa.
Mwenzako akigundua hilo, huo ndiyo utakuwa mwanzo kutafuta njia ya kukuacha.

Makala haya yanawagusa watu wote walio kwenye ulimwengu wa mapenzi ili kujenga uhusiano ulio imara. Jiepushe kujirahisi hovyo, si kwamba unapendwa bali unajishushia heshima yako.

Umeshindwa kabisa kuacha kujichua

Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Najua unaona aibu, hasa kama una tabia hiyo. Usiogope rafiki yangu, leo nitazungumza na wewe taratibu halafu mwisho kabisa nitakuacha na tabasamu la nguvu!

Ndugu zangu, wakati mwingine kuna mambo magumu kidogo ambayo baadhi ya watu wanayaonea aibu, lakini yanaendelea kuwa tatizo kwa watu wengi. Leo tutazungumza. Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo, hawapendi hata kidogo.

Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha, lakini baada ya saa kadhaa kupita, wanarudi kule kule. Kama una tabia hiyo, utakuwa unanielewa vizuri zaidi juu ya kile ninachokizungumzia hapa. Hebu twende tukaone.

KUJICHUA NI NINI HASA?
Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.

Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha!

Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.

INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika.

Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo.

Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.

Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini.

CHANZO NI NINI HASA?
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko.
Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.

Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.

Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa kila kitu kimemalizika. Unajua atakachosema? Sikia: “Mh! Kumbe ndiyo mwisho wake ni hivi? Lakini kama nimesikia starehe hivi...”
Hiyo hutokea pia wakati wa kuoga, ambapo wakati wa kujisugua kwa dodoki, msisimko ukitokea, madhara yanakuwa kama nilivyoeleza hapo juu.

Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta tayari!
Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana.

Sababu nyingine ni kunyimwa au kutotoshelezwa kimahaba na mwenzake.Wengi imewagusa, lakini kuna makundi mawili; wapo waathirika ambao wanatamani kuachana na utumwa huu na wengine wameathirika zaidi, kiasi kwamba hawana mpango wa kuacha.


Wengine wameenda mbali zaidi, kwa vile hawafikirii kuachana na mchezo huu, wamefikia hatua wanasema kwamba hakuna madhara kwa mtu anayejichua! Nimepokea simu nyingi sana, meseji nyingi na wengine wamejadiliana pamoja na marafiki wengine kwenye ukurasa wangu wa facebook.

Watu wanatetea wazi wazi, kwamba kujichua hakuna madhara. Sikia rafiki yangu, hata anayevuta sigara anajua kwamba ina madhara kwa afya yake, lakini ili kujifariji, atajenga hoja kwamba, haimdhuru na badala yake inamsaidia sana kuondoa baridi na haina kilevi.

Wakati mvuta sigara akisema hivyo, mlevi naye atakuja na hoja kwamba, pombe inamsaidia sana kupunguza mawazo. Kila mmoja atatetea upande wake. Ni jambo la kawaida kabisa.

Nikiwa naelekea kuendelea na mada yetu, rafiki yangu mpendwa kama wewe ni ‘muumini’ wa tabia hiyo, unatakiwa kufahamu kwamba unafanya jambo HATARI sana, si tu kwa afya yako, kisaikolojia na dhambi ya uzinifu ambayo hiyo itatokana na uhusiano wako mwema na imani ya dini yako, NDOA yako ipo/itakuwa hatarini.

Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilieleza maana ya kujichua, namna tendo linavyofanyika na jinsi mtu anavyoanza mchezo huo bila kutegemea. Sasa rafiki, hebu tuendelee kwenye namna tatizo linavyokua.

UKUAJI WA TATIZO
Mwathirika akishazoea, hufanya tendo hilo kama sehemu ya maisha yake. Alianza bila kujua matokeo yake, lakini sasa amejikuta akianza kuupenda na idadi ya ufanywaji wa tendo huanza kupanda, baada ya siku tatu, siku mbili, kila siku na hatimaye kwa siku zaidi ya mara moja.

“Kaka Shaluwa, najichukia sana, yaani nimekuwa mtumwa kabisa wa kufanya huu ujinga.
Kwa siku nafanya mara mbili au zaidi, lakini si chini ya hapo,” alisema rafiki mmoja, aliyenipigia simu baada ya kusoma sehemu ya kwanza ya mada hii wiki iliyopita.

Ukweli ni kwamba, mfanyaji kwa vile ameshapata ‘mteremko’ wa kutimiza haja zake, kwanza ataanza kuwadharau wanawake/wanaume, kwamba hawawezi kumtisha, kwa sababu ana njia za kujifurahisha mwenyewe.

Pili, hufikia hatua ya kuwachukia watu wa jinsia pacha, akiwaona kama ‘wanaringa’ hasa kama atakuwa amemshawishi kimapenzi na kukatawaliwa.

ATHARI ZAKE
Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.

Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda za mitaani, zenye utafiti hewa.

Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.


Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika.

Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!

Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.

Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.

“Najuta kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.

“Kuna rafiki yangu mmoja nilikuwa nakaa naye bweni moja alinifundisha. Sikujua kama madhara yake ni makubwa kiasi hiki. Ilikuwa ni shule ya wasichana tupu, kwa hiyo akanidanganya kwamba tuachane na wanaume tujichue...kumbe alikuwa ananisaga!” hii ni sehemu ya ushuhuda mwingine wa mchezo huo.

Athari nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia hapo hapo!

UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.


MFADHAIKO
Mtu ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili.

Si ajabu mtu mwenye mchezo huo, kutembelea akimwangalia mwanamke kuanzia Magomeni hadi Manzese! Amefadhaika. Ameshazoea kumaliza kazi nzima akiwa peke yake, kwa hiyo raha yake inabaki kuwa katika picha tu na si kitu halisi.

Macho yanakuwa juju juu, si kwa kupenda, ni kwa sababu tayari ameshaathiriwa na tatizo hilo. akitoka hapo, ujue moja kwa moja faragha, anaanza mambo yake. Kelele nyingi, kumbe yupo peke yake!

Mfadhaiko hauishii hapo, hata akiwa kwenye vyombo vya usafiri au mkusanyiko wa watu, mwathirika huweza kumaliza ‘kazi’ kwa macho tu, tena wakati mwingine bila kuwa na taarifa. Anakuja kugungua baadaye sana, kwamba kumbe kila kitu kilishafanyika bila hiyari yake.

KUSHINDWA TENDO LA KAWAIDA
Mwenye mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake, anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha. Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza.

Kwanza, anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa tukio lenyewe.

Anakuwa goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza, kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.

Baadhi yao, hubaki wakiwa baada ya wahusika wao kuwagomea katikati ya safari. Zipo athari nyingi zaidi ya hizo, kutegemea na namna tatizo lilivyokomaa na aina ya jinsia.

KUFEDHEHEKA
Baada ya hayo hapo juu kujitokeza kwenye ndoa/uhusiano wa mwathirika, kinachofuata sasa inakuwa ni kufedheheka. Kwa bahati mbaya sana, unaweza kufanya siri mchezo wako, lakini athari zikawa wazi kwa mwenzako.

Hata kama hatagundua chanzo cha tatizo, lakini atagundua kwamba huna msisimko, huwezi kazi au vyovyote vile. Wengi husema kwa hisia, humaanisha kwamba hakuna wanachopata kutoka kwa wenzao, lakini mambo yakizidi kuwa hovyo, wanafunguka: “Mwenzangu kila siku unaniacha na kiu, una tatizo gani?”

Kauli hiyo rafiki yangu, inatosha kabisa kukufanya ushindwe kazi moja kwa moja. Unajua nini? Utaanza kuwaza: “Kumbe siwezi kitu...halafu mwenzangu ameshagundua. Nitafanyaje mimi? Mbona nahadhirika?”

Ndugu yangu, ikifikia hapo utakuwa unamkimbia mwenzako na kwenda chemba kumaliza biashara zako mwenyewe. Furaha ya moyo itatokea wapi? Kama ndiyo mnaishi kinyumba au mpo ndani ya ndoa ndiyo kabisaaa!
Umeona kazi hiyo?

UNATAKA KUACHA?
Hakuwa dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu. Najua wengi walikuwa na hamu ya kutaka kusikia, wataachaje huu mchezo. Ndugu zangu, NI RAHISI SANA, lakini usitegemee Shaluwa atakuwa na mambo mapya sana ya kukufanya uache.

Usitarajie kwamba nitakuja kuingia kwenye nafsi yako na kukuambia ACHA KUJICHUA! Ndugu zangu, nitawapa dondoo chache sana, lakini kubwa ni kwamba ATHARI nilizotaja hapo juu zinatosha kabisa kukubadilisha!

Hebu nikuulize, utakuwa na hamu ya kuendelea na haya mambo kama ndoa yako itakuwa hatarini? Nani atakubali kufedheheka? Nani atakubali kupoteza heshima yake? Bila shaka hakuna. Pitia dondoo zifuatazo;

(i) Badilisha utaratibu wa kulala, lala kifudifudi, badala ya chali (rejea maelezo yangu ya awali kuhusu chanzo cha tatizo)
(ii) Acha kuangalia mikanda ya kikubwa ukiwa peke yako.
(iii) Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi, mazungumzo ya aina hiyo na kampani za watu wanaopenda kusimulia mambo ya faragha.


(iv) Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri.
(v) Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.
(vi) Juu ya yote haya, FUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na ogopa athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA mchezo huo ili kulinda heshima yako na kujipa furaha ya maisha.

Hivi anakutesa au unajitesa mwenyewe?

Wengi wamekuwa wakiumia sana mioyo yao kutokana na ama kukosa penzi la kweli au kuingia katika penzi la kitapeli wakiamini ni penzi la dhati. Tatizo hili limekuwa likiwasumbua wengi, inawezekana hata wewe unayesoma makala haya, limewahi kukukuta au upo katika tatizo hili hivi sasa.

Tatizo hili husababishwa na kukosa umakini ikiwa ni pamoja na kutofuata taratibu sahihi kabla na baada ya kuanzisha uhusiano wa mapenzi. Hapa sasa ndiyo chanzo cha matatizo. Wapendwa wasomaji wangu, unapokuwa na simanzi ni wazi kwamba kila kitu kitakuwa hakiendi sawa, maisha yanabadilika, kila unachokipanga kinavurugika, ufanisi wako kazini unashuka.

Siyo ajabu, bosi wako anafikiria kukufukuza kazi kutokana na kuboronga ofisini. Kimsingi simanzi ni tatizo sugu katika maisha ya kiuhusiano na ni vyema ikiwa umejifunza mapema jinsi ya kuepuka simanzi katika maisha yako ya kimapenzi.
Kuna mambo mengi ambayo wengi huyakwepa ama kwa kuyajua na wakati mwingine bila kujua kuwa wanakosea na mwisho wanajisababishia simanzi ya moyo.

Katika mada hii nitakupa dawa ya kukuondolea simanzi moyoni mwako. Inawezekana umeshakata tamaa, baada ya kuachwa na kila mwanaume unayeanzisha naye uhusiano ukiamini una mikosi, hapo utakuwa unakosea sana, huna balaa wala nuksi ndugu yangu, ni kutojipanga na kutokuwa na utayari wa kukutana na matatizo katika uhusiano.

Hata hivyo, kwa kupitia mada hii kwa makini utaingiza kitu kipya ubongoni mwako na kukufanya uwe mpya katika ulimwengu wa mapenzi.

Kuna wengine wamekuwa wakilia kila siku, inawezekana hata wewe unayesoma mada hii hivi sasa upo katika matatizo makubwa ya kimapenzi na huoni kama kuna sababu ya kuendelea kuishi.

Hapo unakosea sana ndugu yangu, maisha bado yanaendelea, unachotakiwa kufanya ni kujiweka tayari kukabiliana na matatizo yajayo, huku ukihakikisha kwamba huruhusu matatizo ya kujitakia katika maisha yako.

Vipo vipengele vingi sana ambavyo kwa kuvifuatilia kwa makini utaweza kuondoka katika utumwa wa mapenzi unaousumbua moyo wako na kuharibu taratibu za maisha yako.

KABLA HUJAANZISHA UHUSIANO
Kipengele hiki kinawahusu wale ambao bado hawajaingia katika uhusiano. Hapa nitafafanua mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuzingatia kabla ya kuingia katika uhusiano utakaokusababishia matatizo. Hutakiwi kuwa chanzo cha matatizo rafiki yangu.

Hapa ni muhimu sana kwako wewe ambaye unatarajia kuingia katika uhusiano mpya. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba, baada ya kugundua vitu vya kuepuka kabla ya kuingia katika uhusiano itakusaidia kufanya maamuzi sahihi na kuingia katika uhusiano mzuri, wenye mwanga mbele yako.

(i) Tafakari...
Simanzi huletwa na mateso ambayo mhusika huyapata akiwa katika uhusiano ambao hakuutarajia. Hii inamaanisha kwamba ama mpenzi uliyenaye hakupendi au wewe mwenyewe umegundua kwamba humpendi!
Hisia hizi zinatosha kabisa kukuingiza katika simanzi ya moyo. Kugundua kwamba mpenzi uliyenaye hakupendi kwa dhati ni tatizo kubwa sana, maana hapa lazima ataanza kukufanyia vitimbi na kukukosesha raha.

Kitendo cha kuanza kumfikiria au kuwaza juu ya mabaya anayokufanyia ni mwanzo wa wewe kufanya vibaya kazini, kutojijali, kupoteza hamu ya kula na mwisho hata afya yako itakuwa ya mashaka.

Katika kukabiliana na hili ni lazima ufikirie zaidi kabla ya kuingia katika uhusiano na patna mpya. Ukiondoa suala la yeye kukupenda, jiulize je, unampenda? Ni kweli moyo wako umeridhika naye?

Mpe mpenzi wako kile wengine wasichowapa wapenzi wao!

Niseme kwamba mapenzi ni idara ambayo ukiipatia, maisha yako yatakuwa ni ya furaha sana na utatamani kifo kisiwepo ili uishi milele lakini ukikosea kidogo tu unaweza kujikuta ni mtu wa kulia kila siku na wakati mwingine kujuta kwa nini Mungu alikuleta duniani.

Ndiyo maana huwa nasema, fanya maamuzi sahihi kwa kumchagua mtu sahihi ambaye moyo wako unaamini atakupata furaha uliyoitarajia.

Baada ya kumpata mtu huyo, tumia gharama yoyote kumshika vilivyo ili asikuponyoke. Hakikisha unamfanya akuone wewe ni wewe na bila wewe maisha yake hayajakamilika.

Hilo litawezekana kama tu utamjali kwa mambo muhimu ambayo nimekuwa nikiyaandika mara kwa mara kupitia safu hii. Sina sababu ya kuyarudia lakini leo nataka kugusia mambo matatu ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiyapotezea na mwishowe kujikuta wanayachukia mapenzi kwa sababu za kujitakia.

Ukijaribu kufuatilia kwa karibu utabaini kuwa, wapo wanawake ambao wamekuwa wakijitengenezea mazingira ya kusalitiwa bila kujua.

Wapo ambao hawajui nini wawape wapenzi wao ili kuwadatisha, wapo ambao wanajua wanachostahili kuwapa wapenzi wao ila kwa makusudi tu wanaamua kutowapa lakini baadaye wakitemwa wanaanza kulia.

Wanaume wanapenda vitu adimu kutoka kwa wapenzi wao, wanapenda vitu ambavyo wanahisi wenzao hawawezi kuvipata kutoka kwa wapenzi wao. Hivyo ndivyo unavyotakiwa kumpa mpenzi wako ili uweze kumshika.

Ninaposema hivyo simaanishi kwamba unatakiwa kumpa mpenzi wako mapenzi kinyume na maumbile, maana najua wapo ambao wameelekeza mawazo yao huko.

Chondechonde simaanishi hayo jamani.Tena naomba niseme kwamba wanaowapa wapenzi wao mapenzi kinyume na maumbile hawajipendi, wanayachukia maisha yao na wako tayari kwa lolote. Sikushauri kabisa ufanye hivyo kwani ni hatari kwa maisha yako.

Ninaposema umpe mpenzi wako kile ambacho wengine hawawapi wapenzi wao namaanisha mengi lakini haya yafuatayo ni ya msingi;

Utundu na ubunifu
Mapenzi ni utundu na ubunifu hasa unapokuwa kwenye uwanja wa sita kwa sita na mtu uliyetokea kumpenda sana. Onyesha utundu wako wote, tumia akili yako kubuni vitu ambavyo unaamini vitampagawisha mpenzi wako. Kwa kufanya hivyo unaweza kuwa wa kipekee kwake na ataamini amempata mtu sahihi.

Usimbanie
Katika hili naomba niseme kwamba mapenzi ni sawa na chakula. Mwanamke anayempenda mume wake anatakiwa kuhakikisha anampa chakula pale anaposikia njaa. Tena mwanamke huyo atampa chakula kwenye ‘hot pot’ kikiwa cha moto na mume atajisevia kiasi kinachomtosha.

Kwenye mapenzi nako ni hivyo hivyo. Mpenzi wako akihitaji kuwa na wewe faragha usitoe visingizio visivyo na msingi na muwapo faragha mpe uhuru wa kula apendavyo, kwa staili aitakayo ila hakikisha unamzuia asile ‘makoko’ kwani yana madhara kwake na kwako.

Kama utafikia hatua ya kumpa mpenzi wako mapenzi kwa ratiba au kumpa penzi katika mazingira ya kigoigoi, tambua siku zako za kuachwa zinahesabika.

Maneno matamu
Mumeo ni mtu wa kumpa maneno matamu kila wakati, maneno ambayo yatamfanya ajisikie kuwa pembeni yako kila wakati.Wapo wanawake ambao hawako makini katika hili na kujikuta ni watu wa kubwatuka ovyo.

Waswahili wanasema maneno matamu ni silaha katika maisha ya kimapenzi hivyo chuja ya kumwambia mtu wako.

UKIMSALITI MPENZI UTAFAIDI NINI?

KAMA kuna kitu kinachukiwa na wengi katika mapenzi, basi ni usaliti. Ni kilio cha wengi. Vijana kwa wazee, wote hawa hawataki kusalitiwa. Usaliti una maumivu makali. Kiukweli kila mmoja huwa anajisikia vibaya sana anaposalitiwa.

Wengi (hasa wanawaume) baada ya kuwasaliti wapenzi wao huwa na maamuzi mazito sana. Wakati mwingine hufikia uamuzi wa kukatisha uhusiano kwa sababu hiyo. Unadhani ni kwa nini wanachukua uamuzi huo mgumu? Hakuna kingine zaidi ya maumivu.

Leo rafiki yangu, nakwenda kuzungumzia upande wa pili wa maumivu ya usaliti. Unajua kuna watu ambao huumia na kuchukia sana wanaposalitiwa, lakini wao ni wasaliti namba moja. Kwa nini wanafanya hivyo?

Je, kwa kufanya hivyo wanafaidika nini? Hebu nizungumze na wewe rafiki yangu ambaye una tabia hiyo mbaya ya kusaliti, unajisikiaje unaposaliti? Amani? Kuna faida unayoipata kwa kusaliti kwako?

BINADAMU WOTE SAWA
Kuna mambo mengi ambayo mpenzi akifanyiwa na mwenzake lazima ataumia sana. Ingawa kuna mengine yanafichwa au kupasishwa kama sahihi, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba yanaumiza.

Kikubwa ambacho unatakiwa kufahamu ni kwamba maumivu hayo yapo sawa kwa kila mmoja. Haijalishi jinsi, umri, kabila wala dini, maumivu ya mapenzi yote yanafanana. Kufanana huko kunasababishwa na mioyo yote kuwa na nyama!
Kwa sababu mioyo yote ina nyama basi unatakiwa kufahamu kwamba, jinsi unavyoumia wewe moyoni mwako, ndivyo mpenzi wako anavyoumia ikiwa utamkwaza kwa namna yoyote.

VIPI UKISALITIWA?
Unajua kabisa una mpenzi, tena inawezekana wakati mwingine mmeshawahi kuzungumza juu ya kuishi pamoja, lakini bila haya wala aibu, unamsaliti! Kwa nini unafanya hivyo? Kama umeona hana thamani tena kwako, kwa nini unazidi kumpotezea muda?
Unafikiri anafurahia sana wewe kuwa na kimada mwingine huko uchochoroni au unadhani atafurahi siku akijua kuwa una mtoto umezaa nje ya ndoa yako? Nafsi yako yenyewe inakusuta, inajua ni kiasi gani unamkosea mpenzi wako lakini unajifanya kichwa ngumu na kuendelea na uchafu wako. Kwa nini hutaki kubadilika?

Hebu jitoe katika nafasi yako, kisha mfanye mpenzi wako ndiyo wewe, halafu fikiria kama yeye ndiyo angekuwa anakusaliti, ungejikiaje? Lazima utaumia! Sasa kama utaumia kwa nini unaendelea kumfanya mwenzako akose raha?

Lazima uwe na moyo wa huruma, akili yako ifanye kazi ipasavyo na kugundua makosa unayoyafanya kisha kufanya mabadiliko ya haraka. Amini jinsi utakavyoumia kwa kufanyiwa mabaya na mwenzako ndivyo mpenzio anavyoumia kwa mabaya unayoyafanya.
Wengi wamekuwa wakiwasaliti wapenzi wao wakiwa hawafikirii siku ya wao kufanyiwa hivyo itakavyokuwa. Hebu vuta picha, unakwenda nyumbani kwa mpenzi wako, unagonga mlango haufunguliwi!

Lakini baadaye unahisi kama ndani kuna watu, hilo linaingia akilini mwako baada ya kuona viatu vya mpenzi wako pamoja na viatu vingine vya jinsi tofauti ya mpenzi wako. Unaamua kusukuma mlango na kuingia ndani, hamadi! Unakuta mpenzio akiwa anafanya mapenzi na patna mwingine...utajisikiaje?
Mapenzi ya kweli hayaambatani na usaliti. Penzi la kweli lina uaminifu wa dhati, kuchukuliana, kupendana, kusaidiana, ukarimu, huruma na mengine mengi ambayo huyafanya mapenzi yazidi kuwa imara kila siku.

HAKUNA MWENYE HAKI YA KUSALITI
Acha kujiwazia mwenyewe, kujiona wewe pekee ndiye mwenye haki ya kuwa salama katika penzi lako. Chunga nafsi yako lakini wakati huo huo ukiangalia kwa jicho la tatu, nafsi ya mwenzako.

Kila mmoja anaumia anapohisi anasalitiwa, hivi unafikiri ni nani, anayependa kushea mapenzi? Nani mwenye haki ya kumsaliti mwenzake? Kimsingi hakuna. Utakuta mwingine simu ya mpenzi wake ikiita yeye anakuwa wa kwanza kuichukua na kutaka kupokea au kusoma sms, lakini subiri sasa simu yake iite; anakuwa mkali huyo! Acha kujifikiria peke yako.

ZINGATIO LA MWISHO
Siamini kama kuna ambacho sijaandika katika vipengele vyote vinne vilivyopita, lakini hapa nakusisitiza ufanye mabadiliko ya haraka ili mwisho wa siku uweze kuishi maisha mapya, mazuri, yenye mapenzi ya kweli huku moyo wako ukiwa huru.

Hutakuwa na hukumu moyoni mwako, maana utakuwa unamtendea haki mpenzi wako. Lakini kama ukiendelea kumsaliti, ujue wazi kwamba utakuwa unajizidishia maumivu katika moyo wako.

Ukiwa mbali na mpenzi wako, mezea lakini jua unasalitiwa!

Tunapozungumzia uhusiano wa kimapenzi, tunazungumzia watu kuwa pamoja na kushirikiana katika kila jambo linalogusa maisha yao. Hata hivyo, watu wanaweza kutokea kupendana lakini yakajitokeza mazingira ambayo yanawalazimisha kuishi mbalimbali.

Wapo waliooana lakini kazi au sababu nyingine zimewafanya waishi mbalimbali.

Kuna wachumba na wapenzi wa kawaida ambao kutafuta maisha kama vile kazi na elimu vimewafanya waishi maeneo tofauti.

Unakuta huyu yuko Tanga, mwingine yuko Arusha. Huyu yupo Tanzania mwingine yuko Marekani lakini wanapendana na hakuna aliye tayari kumkosa mwenzake.

Katika hili, ninachotaka kukizungumzia ni hii kasi ya wapenzi wanaoishi mbalimbali kusalitiana.

Katika mapenzi ya kweli hakuna suala la kusalitiana, kila mmoja atajitahidi kuvumilia na kuhakikisha anavishinda vishawishi ili asigawe penzi kwa mtu mwingine.

Lakini sasa kuna mazingira flani ambayo yakiwepo kusalitiana kunakuwa na asilimia kubwa kutokea. Juzi nilibahatika kuzungumza na dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Fauzia.

Yeye anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mchumba wake aliyemtaja kwa jina moja la Juma anasoma Uganda.

Dada huyu anasema: “Tulikuwa tunapendana sana, alikuwa ananipa mapenzi ambayo sijawahi kuyapata, aliniahidi ndoa akanivisha pete lakini huku tunakoelekea naona kabisa hatutafikia ndoto zetu.

“Yeye yuko Uganda na mimi niko Dar lakini taarifa niliyopewa na ndugu yangu aliyepo chuoni hapo ambaye hawajuani ni kwamba, mchumba wangu huyu ana mtu mwingine huko na wamekuwa wakionekana maeneo wakiponda raha.

“Naumia sana kwani kila nikimpigia simu na kumuuliza juu ya hilo ananiambia, hayo ni maneno ya watu wasiopenda kutuona tunapendana. Eti ananiambia hana mwingne anayempenda zaidi yangu lakini huku naambiwa ana mtu mwingine.”

Hilo limemtokea Fauzia lakini ninachoamini ni kwamba hayo ndiyo mazingira yanayojitokeza kwa wapenzi wengi wanaoishi mbalimbali. Uvumilivu na uzalendo vimekuwa vikiwashinda wengi.

Mpenzi wako anaweza kuwa mbali na wewe na akakuahidi kutokukusaliti lakini akiwa huko akakusaliti bila hata wewe kujua, lakini watu wanaoujua uhusiano wenu wanabaki kukuonea huruma.

Ni suala lisilo na ubishi kwamba hisia ni kitu kigumu sana kukizuia, unaweza kumuuliza mtu kwamba, anawezaje kukabiliana na hisia zake wakati mpenzi wake yuko mbali?

Jibu atakuambia eti akijiwa na hisia hizo anajiweka bize na mambo mengine.

Ni kweli wapo wanaoweza kufanya hivyo lakini wengi wanaishia kusaliti tena wengine huku mioyo yao ikiwauma.

Mioyo yao inawauma na roho zao zinawasuta kwa kuwa wameshawaahidi wapenzi wao kuwa hawatawasaliti lakini wanafanya hivyo kwa sababu ya tamaa zao.

Usaliti unakujaje?
Kwanza ifahamike kwamba, kama mpenzi wako yuko mbali sana na wewe na mnakaa kwa muda hata wa miezi sita na zaidi bila kuonana, kusalitiwa kuna asilimia nyingi ila unachotakiwa kukifanya ni kumuamini tu mpenzi wako.

Unatakiwa kumuamini tu kwa kuwa, kwanza ni vigumu kubaini kuwa anakusaliti na hata ukimuuliza atakuambia hawezi kukusaliti lakini kumbe inawezekana hata muda huo wakati mnaongea yuko na mtu mwingine kitandani.

Iko hivi, kama mpenzi wako yuko masomoni, elewa huko aliko atakutana na mtu mwingne ambaye naye mpenzi wake hayuko naye.

Hawa wataanzisha urafiki wa kwaida, watapeana kampani za hapa na pale lakini hawa wanayo nafasi kubwa ya kuwasaliti wapenzi wao, na hiki ndicho kinachotoea kwa wengi.

Hilo liko sana vyuoni na makazini hivyo kama mpenzi wako yuko mbali na wewe kwa sababu ambazo hazizuiliki, unatakiwa kuwa na moyo wa uvumilivu au utakiwa kuwa ni mtu wa kupotezea sana laa sivyo unaweza kujikuta unaachana na mtu ambaye ulitokea kumpenda sana.

Kujizuia ni vigumu?
Wapo wanaoweza kukabiliana vilivyo na tamaa zao, hawa ni wale wachache wanaowaheshimu wapenzi wao, wanaoweza kutafuta njia mbadala za kuziridhisha nafsi zao pale hisia za kufanya mapenzi zinapowajia.

Dhana hizi zinawaharibia wanawake kimapenzi

KUNA msemo kuwa: “Wanawake, mwalimu wao ni kipofu.” Mimi siuamini kwa maana umekaa kiukandamizaji zaidi. Haujengi heshima kwa mtu wa jinsi ya kike tangu analizaliwa mpaka anapoingia kaburini. Binafsi naamini wapo wenye uelewa mkubwa lakini wanashambuliwa na mapokeo ya samaki mmoja akioza.

Ni msemo ambao ukiingia kwenye vichwa vya watu unaweza kuwafanya wanaume wawadharau hata mama zao. Mama anatoa mafundisho lakini kijana anasikiliza, linaingilia sikio la kwanza na kutokea la pili. Kichwani anajiongeza: “Aah, hawa si mwalimu wao kipofu?”

Msemo huo unamaanisha kuwa wanawake huwa hawajui waendako. Kwamba njia ya kupita walifundishwa na mwalimu mwenye ulemavu wa macho. Siupendi kwa sababu siyo tu hauna ladha nzuri kwa mwanamke bali pia kwa mtu mwenye ulemavu husika. Unadhalilisha kupita kiasi.

Tangu nikiwa na umri mdogo, nilipenda sana kusikiliza busara za watu walionizidi umri. Niliamini wananijenga na kweli walifanya hivyo. Mtazamo huo, ulinifanya nijue mengi nikiwa na umri mdogo. Hata haya ninayoandika na kushauri, yanatokana na elimu niliyopata kwenye kada tofauti.

Wakati huo sijui ndani ya mwanamke kuna nini, mtu mmoja aliniambia: “Mdogo wangu Luqman, napenda unavyopenda kukaa na sisi wakubwa. Unaweza kuwa na busara katika maisha yako lakini usipokuwa mwangalifu, mwanamke anaweza kukufanya uonekane mwendawazimu mtaani.

“Siku ukiwa na mwanamke, jaribu sana kuwa mwangalifu. Unaweza kumpa kila atakacho lakini mwisho akakuuguza uendawazimu. Ukatembea barabarani unazungumza peke yako kama kichaa au ukiwa nyumbani ukashinda unabwabwaja maneno yasiyoeleweka mpaka majirani wakakuona mwendawazimu.

“Mkeo anaweza kutoka nyumbani anakwenda kumtembelea shangazi yake, kwa kumthamini na kwa sababu huna gari, ukampa fedha ya kukodi teksi. Akitoka njiani, anakutana na dereva teksi anampa lifti. Huwezi kuamini, huyo aliyempa lifti ndiye atamuona bora, mwenye roho nzuri kuliko wewe uliyempa fedha ya kuchukua teksi.

“Matokeo yake ni kwamba akishamuona ni mkarimu sana, anakuwa mnyenyekevu hata kwenye maeneo mengine. Mwisho wanakuwa wapenzi. Hiyo ndiyo tabia ya mwanamke, atasahau mema yako, hatajali watoto mnaolea.” Huyo mtu aliyeniambia maneno hayo anaitwa Jaffari, ni mtu mzima hivi sasa. Enzi hizo nilikuwa nasoma sekondari Mwanza.

Ukweli upo wapi? Ninachoweza kueleza ni kwamba wapo wanawake waungwana mno hapa duniani. Wanadumisha mapenzi ya dhati bila kusaliti licha ya kukumbana na vishawishi kemkem. Wanajua thamani ya wapenzi wao pamoja na changamoto zinazoweza kuwakabili katika maisha.

Hata hivyo, kuna aina ya wanawake ambao Jaffari alikutana nao ndiyo maana akasema hivyo. Isingekuwa rahisi kutoa maneno hayo pasipo kuona kitu. Inawezekana alitendwa na mkewe au alishuhudia kitu kwa rafiki yake, hivyo kumpa tafsiri aliyojijengea kuhusu wanawake.

Tukishika moja kuwa kuna kitu alijionea, basi ni vema kuwazungumzia wanawake ambao walimfanya akawa na mtazamo huo. Hao ndiyo wanaowaharibia wengine mpaka wanakosa thamani. Mtu anatendwa na mkewe lakini lawama anazielekeza kwa wanawake wote kwamba eti ndivyo walivyo!

Jambo ambalo mtu hapendi afanyiwe, basi asianze kumfanyia mwenzake.

Heshima, woga na ‘breki’ katika kauli, vinapaswa kuzingatiwa. Kusaliti maana yake umekosa woga, heshima na busara ya kimapenzi na maisha kwa jumla.

Hekima ni ipi? Kuendelea kuwa na mwenzi ambaye hana heshima juu yako, hakuhofii kwa chochote, wala busara ya maisha haimuongozi kutenda yaliyo mema kwa ajili ya ustawi wa familia yenu. Bila shaka, hekima inafaa kukuongoza kuchukua uamuzi kwa ajili ya furaha na amani ya kudumu baadaye.

Nitoe hoja kuwa hata wanaume wapo wenye matatizo mtindo mmoja, kwa hiyo na wanawake wapo wenye hulka tofauti.

Kama huyo wako ni pasua kichwa, basi wapo waliojaliwa utulivu, heshima, hekima na maarifa ya kudumisha uhusiano. Ikiwa huyo anakunyima furaha, angalia kama unaweza kujivua gamba, kwani wapo wanawake wema.

Mungu hajaumba mtu akamfanya kuwa mbaya kwa asilimia 100, Shetani ndiye anayeharibu vichwa vya watu na kuwafanya wawe na akili zisizofaa. Hata katika jamii ya Wasamaria, alipatikana mmoja aliye mwema ndiyo maana akaitwa Msamaria mwema.

Hivyo basi, wasisemwe vibaya wanawake wote kwa ajili ya makosa ya wachache.

Hata hivyo, hao wachache wanapaswa kubadilika ili wawape heshima wenzao.

Tamaa haifai kwa namna yoyote.

Binafsi nawaheshimu wanawake kwa maana ndiyo waliotufanya tustarehe kwenye matumbo yao kwa miezi tisa, wanawezesha tuitwe akina baba na kadhalika.

Mambo hayo makuu, hayapingiki ndani ya kila mwanaume isipokuwa Adam.

Pamoja na hivyo, zipo dhana nyingine nyingi ambazo zinafanya wanawake wasemwe vibaya. Twende kwa mifano.

Hivi karibuni, niliitwa nimshauri kijana mmoja ambaye kwa hakika alikuwa amechanganyikiwa kabisa.
Alichanganywa na mapenzi.

Mwanamke ambaye aliamini ndiye wa maisha yake, alimuacha katika mazingira ambayo hakuyategemea.

Alikuwa anamhudumia kwa kila kitu lakini akapigwa kibuti kwa SMS.

Kijana huyo anaitwa Mully, akiwa kazini kwake, akaona SMS iliyotoka kwa mtu ‘aliyemsevu’ kwa jina la My Dream.

Kama ujuavyo tena mapenzi, kijana akafungua haraka, akitegemea atapata maneno matamu kutoka kwa mwenzi wake lakini alichokutana nacho ni hiki: “Kuanzia leo, mimi na wewe basi.

Nimepata mchumba nataka kuolewa.”

Mully aliposoma maneno hayo akapagawa, akaamua kupiga simu ya mpenzi wake lakini hakupokea.

Akaamua kumuuliza kwa SMS: “Baby upo serious au unatania?” Haikupita hata dakika moja, majibu yakarudi: “Nipo serious kabisa, tena kuanzia leo usiniite baby na usinijue kwa lolote.”

Meseji hiyo ikamchanganya akili kijana, akaondoka kazini kwake bila hata kuwaaga wenzake.

Yule mpenzi wake anaitwa Janette, ni mtumishi wa ndani kwenye nyumba ya ofisa wa benki Masaki, Dar. Kijana akaondoka kazini kwake Mwenge hadi kazini kwa mkewe. Akili siyo zake.
Itaendelea wiki ijayo

Tunaendelea kuchambua kuhusu dhana ambazo zinawaharibia wanawake kimapenzi. Katika kuhakikisha somo linaeleweka sawia, mwishoni mwa makala ya wiki iliyopita, nilieleza mfano huu:

Hivi karibuni, niliitwa nimshauri kijana mmoja ambaye kwa hakika alikuwa amechanganyikiwa kabisa.

Alichanganywa na mapenzi. Mwanamke ambaye aliamini ndiye wa maisha yake, alimuacha katika mazingira ambayo hakuyategemea. Alikuwa anamhudumia kwa kila kitu lakini akapigwa kibuti kwa SMS.

Kijana huyo anaitwa Mully, akiwa kazini kwake, akaona SMS iliyotoka kwa mtu ‘aliyemsevu’ kwa jina la My Dream. Kama ujuavyo tena mapenzi, kijana akafungua haraka, akitegemea atapata maneno matamu kutoka kwa mwenzi wake lakini alichokutana nacho ni hiki: “Kuanzia leo, mimi na wewe basi. Nimepata mchumba nataka kuolewa.”
Mully aliposoma maneno hayo akapagawa, akaamua kupiga simu ya mpenzi wake lakini hakupokea. Akaamua kumuuliza kwa SMS: “Baby upo serious au unatania?” Haikupita hata dakika moja, majibu yakarudi: “Nipo serious kabisa, tena kuanzia leo usiniite baby na usinijue kwa lolote.”
Meseji hiyo ikamchanganya akili kijana, akaondoka kazini kwake bila hata kuwaaga wenzake. Yule mpenzi wake anaitwa Janette, ni mtumishi wa ndani kwenye nyumba ya ofisa wa benki Masaki, Dar. Kijana akaondoka kazini kwake Mwenge hadi kazini kwa mkewe. Akili siyo zake.
Alipofika, akagonga geti halikufunguliwa, kwa hiyo akapanga matofali getini akakaa. Baadaye Janette akatoka, alikuwa anakwenda dukani, akakutana uso kwa uso na Mully. Yakaanza maneno, baby nimekukosea nini? … sikutaki… baby niambie kosa langu… nimesema sikutaki...
Mtoto wa kike akaona ubishi unampotezea muda, akaingia ndani, akatoka nje na beseni la maji machafu, akamwagia Mully. Kijana wa watu akaloa chapachapa. Janette akarudi ndani, akapiga simu kwa bosi wake, punde polisi wakafika na kumzoa, eti ni mwizi.
Kaka yake Mully akaenda kumuwekea dhamana Oysterbay Polisi. Kuanzia hapo kijana akawa chini, akawa anazungumza hovyo, kazi akawa hafanyi. Kijana akasema: “Mbona mimi ningemuoa tu, sina shida.” Kijana akawa hali, haogi, kazi hafanyi. Akili zikamruka.
Nilijitahidi kumpa ushauri unaofaa kwa vipindi vitatu ndani ya siku tatu mfululizo, baada ya kuona anapata nafuu, nilishauri apelekwe eneo ambalo atabadili mazingira. Alipelekwa nyumbani kwao Singida. Wiki iliyopita, alirudi Dar akiwa mpya kabisa. Anatazama mbele na hamfikirii tena yule mwanamke.
Hata kazi anaendelea vizuri. Machungu ya kuachwa na Janette yamebaki historia. Vema amekaa sawa lakini kitu ambacho kipo wazi ni kuwa Mully alimpenda sana mpenzi wake na aliamini ndiye mwanamke wa maisha. Hali hiyo ndiyo ilimfanya ashindwe kupokea matokeo ya kuachwa.
Alishawekeza mambo mengi kwa Janette hususan rasilimali. Mully aliniambia kuwa kwa siku alikuwa anampa Janette kuanzia shilingi 15,000 mpaka 20,000. Alikuwa anamnunulia mavazi ya kisasa, kiasi kwamba ukimuona, usingeweza kudhani ni mfanyakazi wa ndani.
Baadaye ikaja kubainika kuwa kumbe Janette alipata kiburi cha kuachana na Mully kwa sababu ya bosi wake. Kwamba yule ofisa wa benki baada ya kumuona mfanyakazi wake anameremeta, akaamua kujiweka, binti naye badala ya kufikiria kuwa ni mume wa mtu akakubali.
Wameendelea kuwa na uhusiano lakini za mwizi ni 40, mke akashtukia kuwa anaibiwa mumewe ndani ya nyumba yake. Akamtimua kazi Janette na kipigo juu. Yule jamaa wala hakumtetea ndiyo kwanza akashiriki kusaidia kumtimua. Binti aende wapi? Kazini ameshaharibu, kwa Mully nako alishalikoroga.

Anakupenda au anakutumia?

Zipo nyingi sana, lakini hapa nitakupa dalili kumi ambazo ukiona mwanamke wako anazo ujue hana penzi la moyoni.


ANAKUTEKA
Mwanamke ana haki ya kudeka kwa mwanaume wake, lakini siyo kwa nia nyingine yoyote zaidi ya kunakshi penzi. Huyu hana nia hiyo, anadeka kwa ajili ya kukupagawisha kimahaba ili aweze kuzishika hisia zako sawasawa.

Mchunguze vizuri, utagundua kwamba hata sauti yake anayoitumia kuzungumza na wewe siyo anayotumia akiwa na shoga zake. Anailegeza kwa kuiremba kwa kila hali.

Anataka kukupagawisha. Hiyo ndiyo nia yake, kukupagawisha sana maana yake hutapindua na hutakuwa na wazo la kuwa na mtu mwingine zaidi yake.

ANAPENDA FEDHA
Ni kawaida mwanamke kumuomba fedha mpenzi wake, lakini huyu asiye na mapenzi ya kweli, huwaza fedha mara zote.

Hata kama utazungumza kuhusu kutoka naye katika matembezi, bado ataulizia kuhusu dau lake.

Ana mahitaji mengi. Mwanamke wa aina hii, ukitoka naye nje ya mji au kulala naye hotelini, asubuhi atataka chake! Jiulize ni mpenzi wako au anajiuza? Mbaya zaidi, hata kama utakuwa mgonjwa na amekuja kukutazama siyo ajabu kabisa kukuomba fedha, akiwa na tabia hii ujue hana mapenzi, anataka kukutumia.

HANA HESHIMA
Kwa kuwa hakupendi na wala hafikirii kuwa na wewe katika ndoa, sifa za uanamke hatakuwa nazo. Inawezekana kabisa anazifahamu vizuri sana sifa hizo, lakini hana muda nazo.

Hasikii ukimwambia kitu, mjeuri na wala haheshimu kauli zako.

Kama mpenzi wako, ambaye una malengo naye ya baadaye, una haki ya kumzuia aina fulani ya mavazi, kampani au tabia ambazo huzipendi.

Kwa mwanamke wa aina hii, kumwambia ni sawa na kumruhusu! Mwanamke huyu, neno heshima ni msamiati mgumu sana kwake.

Unajua kwa nini? Kwa sababu hakupendi.

Dalili 4 za mwanaume aliye tayari kwa maisha ya ndoa

Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaume wanaoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuoa kila siku ni wengi lakini je wanaoolewa wote wanaingia kwenye maisha ya ndoa na watu sahihi? Jibu ni hapana, na hii ni kwa sababu wanawake wengine wanakubali kuolewa na wanaume ambao hawakujiandaa kuingia kwenye maisha hayo. Dalili zenyewe ni hizi hapa chini.


Waliobaini kuwa ni muda mufaka
Unaweza kuwa kwenye uhusiano na mwanaume ambaye umri wake umekwenda lakini bado anaona anastahili kuwa kwenye maisha ya ‘ubachela’. Ukikubali kuolewa na mwanaume wa sampuli hii lazima atakusumbua lakini yule ambaye amekaa, akatafakari kisha akagundua kuwa ni wakati muafaka wa kuoa, ni wazi huyo atakuwa amejiandaa na hata ukimkubalia sidhani kama utajuta.

Anajiamini, siyo tegemezi
Ni kweli mapenzi hayana uhusiano wowote na fedha lakini ukweli usiofichika ni kwamba kama mwanaume hana kazi inayomuwezesha kumuingizia kipato, hawezi kuwa miongoni mwa wale wanaostahili kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Ukikubali kuolewa na mwanaume asiye na kitu eti kwa sababu tu umempenda na moyo wako hauko tayari kumkosa, ujue unajiingiza kwenye maisha ya bahati nasibu kitu ambacho siyo kizuri. Kama huyo uliyenaye siyo tegemezi, ni mtu mwenye uwezo wa kukulisha na kukutimizia shida zako zinazohitaji fedha, usione hatari kumwambia afanye hima akatoe mahari muoane.

Anachukua nafasi ya baba
Kuna baadhi ya wanaume licha kwamba hawajaingia kwenye maisha ya ndoa na hawajafanikiwa kuwa na watoto lakini wameshaanza kuzishika nafasi za ‘ubaba’. Unaweza kuwa na mpenzi akawa ni mtu wa kupenda sana watoto na wakati mwingine kuzungumzia namna wa kwake watakavyokuwa. Huyu ni mwanaume ambaye ana dalili za kutaka kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Anakuchukulia kama mke wake
Chukulia kwamba uko na mpenzi wako lakini jinsi anavyokuchukulia ni kama mke wake. Kwa kifupi utaanza kumuona anachukua nafasi ya mume. Kwa mfano ataanza kuweka mikakati kwa ajili ya maisha yenu ya baadae, atakutambulisha kwa ndugu, jamaa na marafiki zake, atakuwa akikushirikisha katika kila suala linalogusa maisha yako na yake.
Aidha, mtaalam wa masuala ya mapenzi nchini Marekani, Carol Morgan anaongeza kuwa, licha ya yote hayo pia mwanaume huyo atakuwa ni mkweli na muwazi katika kila jambo.
Hizo ni dalili nne za mwanaume ambaye amejiandaa kuingia katika maisha ya ndoa.

Njia sahihi za kutatua migogoro ya kimapenzi

Siku hazisimami, daima zinasonga mbele kwa mbele. Mungu ambaye ndiye mfalme wa kila kilichomo mbinguni na ardhini, anawezesha mabadiliko ya kutisha ndani ya sayari ya dunia. Hakukosea Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ alipoimba Siku Hazigandi.

Kwa kila nukta tunayoivuka, mabadiliko yanayotokea, neema zinazotufikia, mitihani inayotukabili, hatuna budi kumshukuru yeye muweza wa yote. Hakika, mimi na wewe binadamu ni viumbe dhaifu, kwa hiyo hatuna ujanja wa kufanya jambo lolote, isipokuwa kwa matakwa yake.

Tunayatazama mapenzi. Tunatoa mada nzuri ambazo lengo lake ni kukuzindua wewe msomaji wangu ili ufanye tafakuri ya kina kuhusu uhusiano wako. Uziangalie hatua zote ulizopita wewe na mpenzi wako kila siku. Naamini kuwa unajifunza na unafanikiwa.

Aidha, shabaha ya kila mada ni kutengeneza mwanzo wa kikomo cha mateso kwenye mapenzi. Hii ni kukuweka sawa, kuangalia machungu ambayo kwa maana moja au nyingine yanakukabili, hivyo ujipange upya, kurekebisha pale ulipojikwaa kisha unafungua ukurasa mpya ambao hautakuumiza tena.


MIGOGORO, neno hili linamaanisha nini?

Tafsiri: Migogoro ni neno linalomaanisha wingi wa mgogoro ambalo linatafsiriwa kama hali ya kutoafikiana baina ya pande mbili au zaidi. Pia inawezekana ikawa ni sura ya fujo.

Tunapoizungumzia migogoro, kwa hali yoyote ile haiepukiki. Na unapoitaja katika uhusiano ni tatizo lisilo na mwenyewe. Maana ya kusema hivyo ni kuwa kila mtu aliye ndani ya ndoa, uchumba au vinginevyo analia kwa staili yake.

Sababu ya kusema hivyo ni kwamba migogoro ni sehemu ya maisha ya kila mtu ambaye yupo katika uhusiano. Kuna usemi wa Kiswahili kuwa vikombe ndani ya kabati vinagongana, itakuwa watu wawili waliopitia makuzi tofauti?

Hivyo basi, usemi huo ndiyo unaothibitisha uwepo wa migogoro katika uhusiano wa kila mtu, ingawa inatofautiana ukubwa kati ya mtu na mtu, kulingana na staili ya maisha ya wahusika.

Sambamba na hilo, jinsi ya kutatua migogoro ni kipimo kingine kinachochangia utofauti kati ya uhusiano wa mtu mmoja hadi mwingine. Inawezekana pia, hasira, busara na ustahimilivu ulionao ukawa chachu ya wewe kutofautiana na jirani yako.

Sababu hiyo, pia inayo matawi mengi, mojawapo ikiwa kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi, au kufikia kipindi ambacho makosa yanakuwa hayagawanyiki huku kila mmoja anakuwa hataki kukubali kosa.

Kimsingi, silaha ya kwanza inayoweza kuuokoa uhusiano wowote ule, ni kwa wapenzi wawili kukubali kuwa na wajibu sawa katika kutafuta suluhu ya migogoro yao. Nafikiri hapo tuko pamoja!

Kikubwa ni kuelewa kuwa ni watu wawili ambao hufanya uhusiano wao uwe wenye afya, pia ni katika idadi hiyo hiyo ambayo husababisha penzi lao lisifike popote. Sababu ni ipi na utofauti huu unasababishwa na nini?

Penzi ni fumbo zito, ndiyo maana huwaunganisha hata wale watu wenye njozi zinazosigana. Inawezekana kicheche akadumu kwenye penzi lake mpaka watu wakashangaa, wakati mtu anayesadikiwa ni mtulivu akawa anahama uhusiano mmoja kwenda mwingine kila siku.

Hata hivyo, muhimu ni kujua mbinu ‘tekniki’ za kutatua migogoro.

Je,Ni sahihi kujiingiza kwenye penzi la muda ‘temporary love’?

Mapenzi ni suala linalotakiwa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa ili yasije yakaleta madhara.
Yawezekana mwaka uliopita ulifanya makosa na ukampa nafasi mtu ambaye mwishoni alikutibulia furaha yako. Usifanye tena makosa!
Chagua mtu sahihi kisha hakikisha unampatia mapenzi ya kweli ili naye aweze kukupatia kile ulichotarajia kutoka kwake.
Baada ya kusema hayo sasa nirudi kwenye mada yangu. Nazungumzia mapenzi ya muda au wazungu wanaita ‘temporary love’. Inaweza ikatokea uko kwenye uhusiano na mtu ambaye ulimuahidi kumpenda daima na kwamba hutamsaliti.
Mpenzi wako huyo mnaishi pamoja lakini sasa inatokea mnatengana kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wenu. Wewe unabaki Tanzania mwenzako anakwenda masomoni Uingereza.
Katika mazingira hayo ni wachache sana wanaoweza kuvumiliana, wengi huwasaliti wapenzi wao kwa kuanzisha uhusiano wa muda na wa siri na mtu mwingine.

Inakuwaje?
Ilishawahi kutokea kwa rafiki yangu, mpenzi wake alipata nafasi ya kwenda kusoma Marekani. Baada ya muda mfupi akaniambia hawezi kukaa bila demu hivyo kuna kasichana kanajua kila kitu kuhusu uhusiano wao lakini kapo tayari kuwa naye kwa muda lakini kwa siri.
Nilijaribu kumsihi asimsaliti shemeji yangu lakini hakunielewa hivyo jamaa akaendelea na yule demu mpaka siku chache kabla ya yule mpenzi wake kurudi, ndiyo wakaachana.
Sasa hivi jamaa anaendelea na mpenzi wake kama kawaida na yule demu aliyekuwa naye kwa muda wanaheshimiana kama dada na kaka.

Nini madhara yake?
Kwanza katika mazingira haya inaonekana huyu mwanaume hana mapenzi ya dhati kwa mpenzi wake na endapo itagundulika kuwa alikuwa na mtu kwa muda, uhusiano wao hauwezi kudumu.
Lakini pia kuna uwezekano mkubwa wa mtu kunogewa. Mwanaume anaweza kunogewa na penzi la yule demu na huenda akabaini kuna vitu alikuwa akivipata kutoka kwake lakini mpenzi wake hana.
Hali hii inaweza kusababisha akamsaliti tena na kama waswahili wasemavyo kuwa muonja asali haonji mara moja, mwisho atachonga mzinga.
Pia watu wanapoanzisha uhusiano kwa muda ni vigumu kuachana moja kwa moja. Kwa maana hiyo mwanaume huyu anaweza kuutibua uhusiano wake kwa penzi la nje aliloonja.

Uhusiano wa muda ni sahihi?
Hauwezi kuwa sahihi hata siku moja na wanaofanya hivyo ni wasaliti ambao wanaweza kujikuta wanajiingiza kwenye matatizo makubwa.
Uvumilivu unatakiwa kuchukua nafasi yake. Kama mpenzi wako yuko mbali na wewe, mtunzie penzi lake. Ukiwa kiruka njia hata kama ni kwa siri Mungu anaweza kukuadhibu na ukajikuta unajuta.

Neno langu
Tuache ulimbukeni kwa kuwa na tamaa za kijinga. Kila unalomfanyia mwenzako kama ni baya jiulize na wewe ukifanyiwa na ukajua utajisikiaje?
Leo hii ukisikia mpenzi wako aliye mbali na wewe kaanzisha uhusiano na mtu mwingine eti kwa kuwa kashindwa kuzizuia hisia zake za mapenzi utajisikiaje?
Huwezi kujisikia vizuri na kama utachukulia poa basi utakuwa huna mapenzi ya dhati kwake.
Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo.

Kabla ya ndoa jiulize, kwa nini umempenda

Uamuzi wa ndoa si wa kujaribu. Unatakiwa kujihakikishia kwamba ni kweli umevutiwa na kila kitu cha mwenzako, kwamba utakuwa naye katika shida na raha. Hayo ndiyo mambo ya kuzingatia.
Nimeshaandika mengi kuhusu sifa za anayetakiwa kuoa au kuolewa, lakini nasogea mbele zaidi na kuangalia sababu za kumpenda mtarajiwa wako katika ndoa.

Zipo sababu za msingi sana ambazo unatakiwa kuwa nazo kabla ya kuingia kwenye ndoa

KWA NINI UJIULIZE
Lazima nifafanue hili kwanza kabla ya kuendelea. Hivi unafikiri ni kwa nini ni lazima kujiuliza sababu za kumpenda mwenzi wako?
Yes! Ni kwa lengo la kujiwekea usalama katika ndoa yako ijayo. Kujiandalia amani na pumziko la kweli. Kwenye mapenzi ya dhati pekee ndipo vinapopatikana vitu nilivyotaja hapo juu.

Kwa maneno mengine kuwa na majibu ya swali linalosomeka kwenye kichwa cha mada hii ni kujihakikishia ndoa bora. Tuendelee kujifunza.

NI MWENZI WA NDOTO ZAKO?
Jambo kubwa kuliko yote ambalo unatakiwa kuliangalia kwa jicho la tatu ni kama mwenzi huyo ni wa ndoto zako. Je, yukoje? Rafiki, siku zote kabla ya kuamua kufanya chochote lazima ujiulize kama ndicho ulichokuwa ukikifikiria.
Hata kwa upande wa mwenzi wako, lazima ujiridhishe, ni kweli ni yule uliyekuwa unamtarajia? Ana sifa unazohitaji? Acha tabia ya kujifariji kwamba utampenda taratibu ndani ya ndoa, hicho kitu hakipo.

Hakuna kujifunza kupenda katika ndoa, lazima ujihakikishie mwenyewe kuwa mwenzi wako ni yule mwenye sifa ulizokuwa ukizitarajia. Hili ni la msingi, maana unaweza kuwa naye siku mbili, ukatamani mwingine nje, kwa nini? Kwa sababu si yule mwenye sifa ulizotarajia.

NI SURA, UMBILE?
Kuna baadhi ya watu utawasikia wakisema: “Mpenzi wangu ananivutia sana, yaani ni mzuri sana. Najua hata nikitoka naye, marafiki zangu watanisifia kwa kuchagua vizuri...”
Hizi ni fikra potofu ndugu zangu. Mapenzi ya kweli hayapo kwenye sura wala umbile la mtu. Vipo vigezo vya muhimu kabisa vya kuzingatia tofauti na uzuri wa sura.

Sura hubadilika ndugu zangu, binadamu wanazeeka, kuna kuugua na matatizo mengine ambayo yanaweza kubadilisha mwonekano ambao ulikuvutia. Je, yakitokea ndiyo utakuwa mwisho wa kumpenda?
Kama leo hii unamuoa kwa sababu umevutiwa na matiti yake madogo, akishazaa na kunyonyesha kisha yakaanguka, ndiyo mwisho wa kumpenda? Umempendea ngozi yake nyororo, akipata ‘aleji’ ya mafuta, ngozi ikaharibika na kuwa na mabakamabaka utakuwa mwisho wenu?

Wewe mwenye mpango wa kuolewa na mwanaume mwenye kigezo cha kifua cha kimapenzi, kesho akifutuka na kuwa na kitambi utamuacha? Rafiki yangu, kiukweli ni kwamba kigezo cha uzuri wa sura na umbile si sahihi kabisa katika kuchagua mwenzi. Vipo vitu vingine muhimu zaidi vya kuangalia.

Kama ulikuwa unaishi katika dunia ya fikra hizo, hama ndugu yangu.

Unajua Kwamba unaweza kuwa chanzo cha maumivu yako

Kama bado hujaingia kwenye ndoa, huu ni wakati wako sahihi wa kufanya uchaguzi bora ambao hautakuwa na majuto hapo baadaye. Hapa nazungumzia juu ya kutizama maisha yako yajayo.
Acha kuangalia leo, wakati kesho yako inaonekana wazi kuwa mbaya yenye majuto ya kila aina. Hapa nitachambua kwa mapana mambo mawili makubwa; Hisia na maisha!
Wapo rafiki zangu ambao wanakubali kuongozwa zaidi na hisia huku wakiacha maisha yao ya baadaye yawe mabaya. Ieleweke kwamba, maisha utakayoishi kesho ni matokeo ya jinsi unavyoishi leo.
Wakati mwingine mtu anakuwa na mpenzi wake, ana kasoro kibao, kila siku ugomvi, hakuna maelewano, lakini kila anapotaka kuachana naye, hisia kali za mapenzi dhidi yake zinamzidi na kujikuta akiendelea kuwepo kwenye penzi la mateso.
Huu si wakati wa kunyanyasika katika mapenzi, ni muda ambao unatakiwa kuangalia vyema tabia na mienendo ya mpenzi wako. Kama hairidhishi, usijiumize; Chukua hatua ya moja kwa moja huku ukizingatia kwamba, maisha yako yanayofuata yatakuwa bora ukijivunia ujana wako.

Hata kama unampenda sana, anajua mapenzi sana, ana faida gani kama kila siku ameendelea kukuumiza? Kukunyanyasa? Kukusimanga? Haoni faida yako, anakudharau waziwazi! Kwa nini uendelee kukaa kifungoni wakati kuna njia?
Mwamuzi wa maisha yako ni wewe, hatatokea mtu wa kukupangia maisha bora hapo baadaye, yote hayo unapaswa kufanya mwenyewe. Chagua maisha unayoyapenda.

Nina maana gani ninaposema maisha? Rafiki zangu, huu ni mustakabali wa maisha yanayofuata. Kwamba maisha yako baada ya leo ni yapi? Unahitaji kuishi maisha gani?

Maana kama ukiwa hujui unataka kuishi vipi, utakuwa unakwenda bora siku zisogee na mwishowe utajikuta ukiingia kwenye majuto. Kwa nini uingie kwenye majuto wakati unaweza kujipanga na kufanya kesho yako iwe bora zaidi?
Ndugu zangu, ninapozungumzia kuhusu hisia nina maana kubwa sana. Kwanza, fahamu kuwa hisia na mapenzi ni vitu viwili tofauti kabisa, ingawa ili uwe na hisia lazima pia uwe na mapenzi.

Kwa maneno mengine, mtu mwenye mapenzi ya dhati ni rahisi zaidi kuongozwa na hisia kuliko mwenye hisia kupanda mbegu ya mapenzi ndani ya moyo wake. Hisia katika mapenzi, tunaitafsiri kama ile hali ya kuingiwa na mapenzi ndani ya moyo kupitiliza, pia kuzama katika penzi kiasi cha kuwa mpofu wa kutoweza kuona mbadala wake.

Mtu mwenye hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wake, huwa haamini kama kuna mwingine ambaye anaweza kuwa kama mpenzi wake, hali hii inasababisha kufunika makosa au matatizo yatakayotokea katika uhusiano wao hata kama ni makubwa.
Akibahatika kugundua, basi uulizaji wake unakuwa si wa kujiamini sana, lakini pia ni mwepesi wa kuyumbishwa au hata kuomba msamaha kwa kosa ambalo ni la mpenzi wake. Huyu tunamwita anayeongozwa na hisia.

Mtu mwenye hisia zaidi kuliko mapenzi, yupo tayari kuishi maisha ya kubahatisha bila kuwa na mipango ya mbele, lakini awe na mpenzi wake. Huu ni ulimbukeni wa hali ya hali juu. Rafiki zangu, kifungo si lazima upelekwe gerezani, hata wewe unaweza kujiingiza katika kifungo cha mapenzi.

Usikubali kuendelea kuwa katika mapenzi na mtu ambaye unajua wazi ana kasoro kibao, kwa sababu eti unampenda! Hata kama unampenda kwa kiwango gani, lakini ndiyo hivyo si mwaminifu, mkorofi, hana heshima; Utaendeleaje na mpenzi wa aina hii?

Lakini katika yote hayo, tatizo kubwa zaidi ambalo ni la hatari, ni ile hali ya kuwa na mwenzi ambaye si mwaminifu. Kutokana na kigezo chako cha kuangalia jinsi hisia zako zinavyokuongoza, wakati mwingine unaweza kusalitiwa lakini usijue au unajua lakini unaamua kuacha kwa kuhofia kumpoteza. Huu ni ulimbukeni rafiki zangu.

Katika suala la usaliti ni vizuri kuwa makini katika kufanya uchunguzi kwanza kabla ya kufanya maamuzi. Mathalani mpenzi wako amekuja, anaonekana amechoka-choka, hana furaha na uso mng’avu kabisa!
Tabasamu lake halipo na kwa kumwangalia tu usoni unagundua kwamba ana alama ya busu kwenye shavu lake! Wakati mwingine ananukia manukato ambayo siyo aliyoyatumia asubuhi.

Au anaweza kuja na furaha kupitiliza, uchangamfu kupitiliza, kukukumbatia kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida ambavyo mmezoeana n.k.
Hizi ni dalili za wazi kabisa, katika hali kama hiyo lazima uwe na mashaka na inawezekana akawa ametoka kwa mtu mwingine. Alama ya busu shavuni mwake, haina haja ya kuwa na maswali mengi maana tayari jibu utakuwa nalo.

Mambo ya Kuzingatia Katika Mapenzi

Uaminifu:
Katika maisha ya uhusiano, mpaka mnaamua kuwa wawili ina maana mmekubali kwa ridhaa yenu. Mmewaacha wengi na kuamua kuwa pamoja, hivyo mnatakiwa kulilinda penzi lenu kwa kuwa waaminifu.

Tabia nzuri:
Hii ndiyo inayobeba uwakilishi wa mwanadamu ndani ya nyumba, ndiyo nguzo imara ambayo itakufanya usimame popote kwa kujiamini.
Katika hili wengi hukosea wanapojiona wana sura na umbile zuri au fedha, basi huanza kuwanyanyasa wenzao kwa kujivunia walivyonavyo na kusahau hakuna kiumbe kilichoumbwa kwa ajili ya kukasirishwa.
Mara nyingi uhusiano wa watu huvunjika kutokana na tabia ya mmoja kuwa mbaya isiyovumilika.

Huruma:
Ndani ya uhusiano, huruma ni kitu muhimu sana, ukiwa nao, huwezi kumuumiza mwenzako.
Nyumba yenye huruma kwa wapendanao hudumu milele na kutenganishwa na kifo. Asiyekuwa na huruma, hufanya jambo lolote bila kujali maumivu ya mwenzake.

Upendo:
Huu ndiyo unaobeba kila kitu kwa vile mwenye upendo ana huruma, ni mvumilivu na tabia njema ndiyo asili yake. Wote mkiwa na upendo hata familia yenu itakuwa yenye tabia nzuri.
Hapa mara nyingi kumekuwa na tatizo kwa baadhi ya watu kuchagua watu hasa wanawake kuchukia ndugu wa mume na mwisho wa siku ndoa huvunjika.

Uvumilivu:
Huu ndiyo muhimu katika maisha yetu ya kila siku, wengi wasio wavumilivu, wamekuwa wakitengana na wenzao. Kuna vitu ambavyo tunatakiwa tuvumiliane kwa vile wanadamu ni viumbe wenye upungufu.
Kukosana ni sehemu ya maisha, lazima mvumiliane, mtangulize kusameheana na kuyasahau yaliyopita. Yapo ya kuvumilia, lakini si yaliyovuka mipaka kwa mtu kushindwa kujirekebisha.

Jifunze lugha za mapenzi

Hakuna linalouma moyo kama mtu kuachana na aliyempenda. Moyo husafiri kilometa nyingi kwa kuwaza. Hakukosea aliyesema sikitiko la mahaba linashinda msiba. Lakini yote hayo yanaweza kuepukika na kukaa mstari ulionyooka endapo mawasiliano yatabeba umuhimu unaotosheleza na kusimama kwenye nguzo zake kuu.

MAWASILIANO: Ni nguzo kuu ya uhusiano. Ikiimarishwa huchochea amani ya kudumu lakini kinyume chake ni kichocheo cha wapenzi kuachana. Ni vizuri kujifunza lugha inayoweza kukufanya uelewane na mwenzako. Sauti yako ukiwa mtaani itofautiane na ile ambayo unaitumia chumbani.

Pengine una kawaida ya kutoa majibu ya mkato unapokuwa unazungumza na rafiki zako, lakini tabia hiyo hutakiwi kuizoea pale unapokuwa na mwenzio chumbani. Ikiwa umezoea kuwaita wenzako: “Wewe!” Mwenzi wako hutakiwi kumwita hivyo.

Ni elimu ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwamba kutofautisha maeneo ni jambo la busara. Kwamba sura yako iwe nyingine unapokutana na watu wa mitaani, itofautiane unapokuwa na wazazi, vivyo hivyo pale ambapo upo sehemu ‘spesho’ na mwenzi wako.

Lazima uwe unabadilika kama kinyonga. Ukiwa kazini mbele ya watu unaowaongoza unazungumza kwa sauti ya amri, lakini hiyo hupaswi kuitumia unapokuwa na wazazi wako. Unaongea kwa sauti kali ya kuamrisha mbele ya baba yako, hiyo adabu umefundishwa wapi?

Kuna lugha ya kuzungumza ukiwa na mwenzi wako. Ni mwiko kutoa sauti ya kuamrisha. Ni vizuri kumnyenyekea lakini si katika kiwango ambacho kitakufanya uonekane una kasoro za kisaikolojia. Tawile kwa kila linalosemwa na mpenzi wako hairuhusiwi, unatakiwa kuweka mbele hisia zako.

Upole kupitiliza hauna maana kwamba wewe ni mpenzi sahihi. Eti, utaonekana una nidhamu na unamsikiliza vizuri mwenzio, la hasha! Utatambulika kuwa mtu hai kulingana na jinsi akili yako inavyofanya kazi. Namna hisia zako zinavyoonesha uhai unapoguswa na matukio mbalimbali ndivyo na ubinadamu wako unavyosomeka.

Unahoji mambo kwa sauti yenye ujazo wa kutosha, unachukia pale unapoona mambo hayajaenda sawa, unaumia pale unapotendwa na unafurahi mipango inapokuwa chanya. Hii ndiyo mantiki ya kukutaka uwe na akili hai. Itashangaza umepata habari kwamba mwenzi wako yupo gesti na mpenzi mwingine halafu utabasamu.

Sumu hatari inayosababisha mmomonyoko wa ndoa au uhusiano wa kimapenzi kwa watu wengi ni kushindwa kujipanga kimaeneo. Ratiba za ofisini kuingiza nyumbani. Marafiki kuathiri taratibu za mapenzi yenu, ingawa kila kitu kina umuhimu wake kulingana na wakati husika.

Umeudhiwa na wafanyakazi wenzako kazini, unatakiwa kuweka hekima mbele. Unarudi nyumbani ukiwa na imani kwamba huko utakutana na mwenzi wako na ndiye mfariji wako. Kichwa kizito, basi mueleze mwenzio ajue kinachokusibu kuliko kumpa majibu ya mkato. Itakuharibia badala ya kukusaidia
Ninachosisitiza hapa ni kuwa uhusiano wa aina yoyote unadumishwa na mawasiliano.

Lugha yako mbele ya mwenzi wako ina nafasi kubwa ya kukufanya uendelee kufurahia penzi lake. Kinyume chake unaweza kujikuta ni kero kwake. Atakuvumilia mwisho atachoka kwa sababu hujui kubembeleza, unapenda kuamrisha.

Unataka kuwa mtu bora kwenye uhusiano? Zingatia chachandu zifuatazo:

TAMBUA MAKOSA YAKO
Hii ni lugha nzuri mno kwenye mapenzi. Unatakiwa kutambua makosa yako haraka na kutafuta njia ya kusuluhisha. Ukijielewa kwamba umekosea halafu ukakaa kimya hutoa ishara mbaya mbele ya safari.

KUWA MWEPESI KUSEMA SAMAHANI
Kiingereza kinatawala sehemu kubwa ya mawasiliano ya Watanzania, kwahiyo ukiona samahani utaonekana upo kienyeji, basi sema I am sorry. Hii ni baada ya kutambua makosa na unapoomba msamaha umaanishe kutoka moyoni.

USINUNE AKINUNA
Ni lugha ya mapenzi kwamba mwenzako akinuna, wewe jishushe ili mpate muafaka. Nyote mkigoma mtafika saa ngapi? Ni kosa kubwa unapobaini mwenzi wako ana hasira, nawe ukapandisha jazba kwani ni kiashiria cha kuachana.

CHUKIA ASIYOYAPENDA
Inafundishwa kwamba rafiki wa rafiki yako ni rafiki yako. Adui wa rafiki yako ni adui yako. Rafiki wa adui yako ni adui yako. Adui wa adui yako ni rafiki yako. Falsafa hii ikupe somo kwamba hutakiwi kupenda yale ambayo anayachukia.
Haikubali mtu ambaye hana jema kwa mwenzi wako, wewe umfanye rafiki. Fikiria upande wako kwamba kuna mtu anakula yamini kukumaliza, halafu ugundue kwamba mpenzi wako huwa anaketi naye na kuzungumza kwa kugongeshana mikono? Heshimu hisia za mwenzako.

ONGEZA MAPENZI KWA ANAYOPENDA
Mapenzi ni sanaa, ukiweza kucheza karata zako mtadumu bila kuchokana. Umeweza kuchukia yale ambayo hayapendi, sasa ni vizuri kuongeza mapenzi kwa yale ambayo anayapenda. Hii itasaidia kuwafanya muonekane ni kitu kimoja daima.
Hata hivyo, iga kwa mambo mazuri, isije ikawa mwenzako ni mtu wa baa kwa sana halafu na wewe umuige. Anapenda siasa, mpe ushirikiano nawe uipende taratibu. Mpira nenda mkaangalie pamoja, muvi na mengineyo, hayo ndiyo mapenzi.

MFANYE AKUTAMANI MUDA WOTE
Ni rahisi, unapokuwa naye muoneshe mapenzi ya dhati. Hakikisha hakasiriki mkiwa pamoja, yanayomhusu unabeba kama yako. Humkaripii na unamfanya yeye ni bora. Msifie kwamba ni mzuri na umueleze kwa hisia jinsi unavyomkubali. Hiyo itamfanya ajenge imani kubwa kwako na ukiwa mbali atajiona pungufu.

USITHUBUTU KUPAYUKA
Hata kama mmegombana, linda sauti yako. Tumia hekima na myamalize kimyakimya.

SWEETHEART, DARLING, BABY, HONEY, DEAR
Mpe heshima yake na umuoneshe ni kwa kiasi gani alivyo na nafasi kubwa kwako. Usipende kumuita kwa kumtaja jina lake au wengine wakishapata mtoto ndiyo utasikia “Mama Chausiku!” au “Baba Semeni!”
Haifai, tumia majina hayo au ukiweza tumia mengine yenye mvuto. Ikupe raha kutamka na yeye imfanye afurahi kusikia kutoka kwako. Mapenzi ni rahisi, utundu kidogo utakufanya uone dunia yote unaimiliki wewe.

Je, Unamuadhibu mpenzi wako kwa kumnyima penzi

Kwa wapenzi kukoseana ni kitu cha kawaida na mara nyingi linapotokea hilo cha msingi ni kusameheana kisha kuyaacha maisha yaendelee. Kwa wengine hali ni tofauti, unamkuta mtu katibuana kidogo na mpenzi wake, anachokifanya ni kusitisha penzi kwake.

Hivi karibuni mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sarafina aliniambia jambo la kusikitisha sana na kama wewe ni mmoja wa watu walio kwenye ndoa au unayetarajia kuingia kwenye maisha hayo, naamini utajifunza kitu.

Mama huyo mkazi wa Kimara jijini Dar anasema: “Mume wangu hivi karibuni alichukua simu yangu na alipoipekua alikuta sms ya mwanaume ambaye kusema ukweli simjui.

“Inavyoonekana huyo jamaa alikosea namba na alikuwa akimtumia mtu wake akimwambia kuwa amefurahishwa na mapenzi aliyompatia jana yake. Nilijitahidi kumwambia mume wangu kuwa huyo mwanaume simjui lakini aling’ang’ania kuwa namjua.

“Nilimsihi asinihukumu kwa kwa kosa ambalo sijalitenda lakini hakunielewa na hapa ninapoongea nina wiki sijakutana naye faragha. Anachelewa kurudi nyumbani na akija nikimwambia ‘nimemmisi’ anakuwa mkali.”
Maneno ya Sarafina yaliniumiza sana na nikaona sehemu ya kuweza kulizungumzia hili ni hapa kwenye mashamsham. Kwa kweli kukoseana tunakoseana lakini ifike mahali linapotokea tatizo kwa wawili waliopendana, ufumbuzi upatikane haraka na isifike hatua ya kununiana na hata kunyima ‘chakula cha usiku’ bila sababu za msingi.

Wapo wanandoa ambao wakikoseana kidogo tu adhabu ni kunyimana penzi, jamani hivi hamjui unapomnyima mpenzi wako haki yake hiyo unamsukuma kukusaliti? Wangapi leo hii wamesababisha waume zao kutafuta nyumba ndogo baada ya kunyimwa vile walivyostahili kupewa na wake zao?

Jamani ifike wakati tuwe makini na maamuzi tunayoyachukua, tusichukue yale ambayo yatatufanya tujute. Hebu jiulize leo unambania mumeo chakula cha usiku eti kwa sababu tu hali ni ngumu, hakuacha fedha za kutosha kwa matumizi, hivi ukimkuta katulizwa na mwanamke mwingine utajisikiaje?

Makala haya yawe fundisho kwako, kosa dogo lisiwe sababu ya kunyimana penzi, ombaneni msamaha yaishe na muendelee kupeana raha. Tabia ya kunyimana inaweza kuleta madhara makubwa kwenye uhusiano wako na ukajuta.

Anakupenda lakini anakutesa, mapenzi yapo wapi

Mtu anasema kuwa ana mpenzi wake ambaye wanapendana sana lakini sasa hivi hamuelewi baada ya kuona upendo umepungua.
Ukiangalia kichwa cha habari hapo juu, kina jibu la moja kwa moja lakini ni vigumu mtu kuelewa kwa vile bado hajifahamu katika mapenzi amesimama upande gani.
Unasema wewe na mpenzi wako mnapendana sana, lakini sasa hivi mpenzi wako humuelewi, ukimpigia simu hapokei kama zamani au akipokea, anakuwa na majibu ya mkato tofauti na mwanzo wa mapenzi yenu.
Hili swali naweza kusema limekuwa fasheni katika mapenzi ya sasa, hasa kwa wapenzi waliokuwa pamoja na baadaye kutengana kwa ajili ya kazi au masomo, kwa hawa lazima baada ya muda tatizo hili hutokea.

Kuna nini?
Wengi sehemu hii huwashinda kwa vile huwa na mapenzi ya mdomoni na machoni. Wapenzi wengi huwa na heshima na uaminifu kama wanawaona wapenzi wao kila siku, mtu huogopa kufanya usaliti kwa kuwa mpenzi wake yupo, lakini huyohuyo huwa hana uaminifu anapokuwa peke yake sehemu ya mbali.

Huwa mwepesi kuanzisha uhusiano mpya kwa kuamini ni wa kupita.
Kwa vile wengi hawana mioyo migumu ya uvumilivu, hujikuta wakizama moja kwa moja na kuwasahau waliowaacha nyumbani. Hapo ndipo ule utata unaosumbua huanza. Utasikia nipo bize au simu kutopokelewa kabisa na kwa wengine huwapa wapenzi wao wapya wapokee.
Kwa vile uliye mbali na mpenzi wako hujui mwenzako kazama kwenye penzi jipya, hapo ndipo huanza kuumia moyoni ukiamini kabisa mpenzi wako anakupenda lakini hujui tatizo.
Kama ungekuwa mfuatiliaji mzuri wa makala zangu, ungejua mtu mwenye mapenzi ya kweli yupo vipi. Mwenye mapenzi ya kweli ni tulizo la mawazo ya mpenzi wake, ni mpole na mwenye huruma na mara zote hujiepusha kuwa sehemu ya maumivu yako.

Hivyo, ukiona mpenzi wako haeleweki, unatakiwa kuanza kuizoea hali ile ili kujiandaa kwa penzi jipya, kwa vile ule mche wa mapenzi ulioupanda ndani ya moyo wa mwenzako umesinyaa.
Usipende kujitesa kwa kujitakia, kama umeona kabisa kuna mabadiliko ndani ya penzi ni wakati wa kuchukua uamuzi mgumu ili kunusuru mateso yasiyo na sababu.

Jiepushe kuishi mapenzi ya mazoea kwa kuamini unapendwa wakati unateswa, hakuna upendo wa mateso hata siku moja. Mapenzi ni furaha na wala si karaha. Acha kuusemea moyo wa mwenzako kuwa anakupenda wakati ndiye chanzo cha ugonjwa wako wa moyo.
Kabla ya kuchukua uamuzi mgumu wa kuvunja penzi, msomee mpenzi wako mashtaka na kumueleza ukweli kuwa umechoka kuumia, akikosa utetezi unaoeleweka, una nafasi ya kuvunja penzi.
Kama atakuwa tayari kukiri makosa na kujirudi, unaweza kumpa nafasi nyingine lakini akirudia makosa, achana naye, fungua ukurasa mpya.

WANAUME TUSIWALAZIMISHE WAKE ZETU KUWA NA ‘VIDUMU’

KATIKA mapenzi ya sasa, mahaba ‘chakula cha usiku’ yanapewa nafasi kubwa sana katika kuleta furaha kwa wawili waliotokea kupendana kwa dhati.
Asikuambie mtu, kumnyima mpenzi wako penzi wakati anapolihitaji unamuumiza kuliko maelezo na anaweza kufikia hatua ya kuhisi humpendi. Atafikiria hivyo kwa kuwa umemnyima raha aliyotarajia kuipata kutoka kwako.
Hapa tunatakiwa kufahamu tu kwamba, furaha ya maisha ya binadamu yeyote inakamilika kwa kuwa na mtu mwenye mapenzi ya dhati kwake na akapatiwa kila alichotarajia yakiwemo ‘mahabati’.
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka tatizo la baadhi ya wanawake kulia kunyimwa ‘mambo’ na waume zao. Mfano wa wanawake hao ni Jastina wa Morogoro ambaye anaeleza kuwa, amefikia hatua ya kutaka kumsaliti mumewe kutokana na kutotimiziwa haki yake hiyo ya ndoa.
“Mimi ni mwanamke bwana, nina hisia na kuna wakati najisikia kabisa hamu ya kukutana na mume wangu faragha lakini sasa mume wangu akirejea nyumbani na nikamwambia kuhusu hilo, anakuwa mkali, eti kachoka!
“Ingekuwa ni siku moja moja sawa lakini yeye kila siku akirudi anakula, analala tena anageukia huko… inakuja kweli? Hivi na mimi nikisema nitafute kidumu changu cha kuniliwaza pale ninapojisikia nitakuwa nakosea?” alilalamika mama huyo.
Malalamiko haya yanaingia akilini licha ya kwamba mawazo aliyonayo Jastina ambayo naamini wapo wengine walio katika mazingira kama hayo siyo sahihi. Mke ana haki ya kupewa ‘chakula cha usiku’ na kama kuna sababu za msingi ni suala la wawili kuzungumza na kuafikiana.
Kitendo cha mume kumbania penzi mkewe kwa maelezo kwamba amechoka kutokana na kazi za kutwa nzima kinaweza kuchangia usaliti katika ndoa.
Najua katika maisha ya sasa watu hasa wanaume wanatumia muda mwingi sana kusaka fedha kwa kufanya kazi na mwisho wake wakirudi nyumbani wanakuwa wamechoka kiasi cha kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi. Lakini sasa ni sahihi kwa wanandoa kukaa muda mrefu bila kupeana mambo? Jibu ni hapana!
Kama ni hivyo, nawashauri wanaume wanapofanya kazi wakumbuke kuna wake zao wapendwa wanawasubiri nyumbani. Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake licha ya kwamba kazi nayo ina umuhimu wake.
Pia kuna jambo ambalo wanaume na hata wanawake hawalijui vizuri, hili ni lile linalohusu mazoezi. Unapofanya mazoezi unawezesha damu kuzunguka na kufika sehemu zote za mwili kwa kiwango kinachotakiwa.
Kukaa ofisini kutwa nzima na kurudi nyumbani na kukaa kwenye kochi kisha kuangalia TV siyo aina ya maisha inayoshauriwa tuishi. Mwili unapochangamka kwa damu kufika kila mahali kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa ‘chakula cha usiku’ na kukipokea huwa kubwa.
Lakini wanawake nao kuna wanaoishi kizamani sana. Hawa ni wale wanaosubiri waume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata mwaka watakaa wakilalamika kwamba hawapati ‘chakula cha usiku’.

Je.Umekata tamaa ya kupata mwenzi wa maisha

KATI ya vitu muhimu katika maisha ya binadamu ni pamoja na ndoa. Ni tendo la muunganiko ambalo linaongeza thamani, heshima na utu mbele ya jamii inayokuzunguka. Wengi wanatamani sana kupata wenzi.
Pamoja na ukweli huo, zipo changamoto ambazo husababisha kuchelewa kupata au kumpata mbabaishaji ambaye hana lengo la dhati.
Wapo wasichana warembo, wanaume watanashati sana, lakini kila wanapokuwa kwenye uhusiano, wanagundua kwamba wapo na watu ambao ‘bado wanazuga’. Hawana mpango wa kuingia kwenye muunganiko wa ndoa.
Hapo ndipo panapotokea kuachana. Rafiki yangu, kuacha, kuacha au kuachana mara kwa mara, kunasababisha sononeko la moyo. Kunakaribisha simanzi na mwisho wake, mhusika hukata tamaa ya kupata mwenzi wa maisha.
Inawezekana kabisa, hata wewe uko kwenye kundi hili. Aaaah! Usihuzunike, anza sasa kutabasamu, maana unakwenda kukutana na dawa baada ya kumaliza kusoma mada hii.


ANZA KUJIJALI
Maumivu ya kuachwa kila wakati, yanaweza kusababisha kutokujiweka ‘sopsop’, kitu ambacho ni tatizo kubwa sana. Sahau maumivu yote, angalia maisha yako yajayo. Rafiki yangu, hivi unadhani kama hujipendi, hujithamini nani atakupenda?
Ninaposema ujipende namaanisha ujipe upendo ule wa kawaida wewe mwenyewe kabla ya kuhitaji upendo wa mtu mwingine. Mwingine inawezekana hajitunzi, anavaa nguo chafu, hapigi pasi, nywele zipo timtim n.k
Nani atakupenda kwa misingi hiyo? Hakuna anayependa kuwa na mtu ambaye hana desturi ya usafi, kwanza hata kama ni mzuri kiasi gani unapokuwa upo rafu, hakuna mtu ambaye atausumbua moyo wake kuanza kukufikiria wewe usiyejipenda.
Siyo lazima wakati wote uwe ‘smati’, kwa kuwa inawezekana wengine wanafanya kazi ambazo zinawalazimu kuvaa nguo chafu, lakini baada ya hapo, unatakiwa kuwa katika hali ya usafi.
Upande wa wasichana siyo lazima uweke nywele zako dawa au usuke rasta wakati vitu hivyo huna uwezo navyo, unaweza ukasuka nywele zako vizuri au wakati mwingine ukanyoa mtindo mzuri unaokubalika ambao hautakuweka katika mtazamo mbaya kwa jamii.
Anza kujipenda kabla ya kuhitaji upendo kutoka kwa mtu mwingine, hiyo itakusaidia kuwa na mvuto na mwonekano mzuri kiasi cha kuweza kumpagawisha mtu mwingine kuanza kuhisi cheche za moto wa mapenzi katika moyo wake.
Safiri na neno hili, huhitaji tena mateso katika maisha yako. Sawa jamani? Haya, tuendelee.

KUJIAMINI NI MUHIMU
Hili ni tatizo la kisaikolojia zaidi kwa sababu kuna baadhi ya watu wanakosa kujiamini. Kuna mwingine anaweza akakaa kwenye kioo kwa saa kadhaa na kuanza kujitoa kasoro katika mwili wake.
Hujiona mbaya asiyevutia na ambaye hana thamani kabisa katika ulimwengu wa mapenzi, hujiona hawezi kupata mpenzi katika maisha yake yote baada ya kujitoa kasoro hizo. Mwingine hujiona ana matiti mabaya, mfupi sana, mrefu sana ana matege, ana makengeza na kasoro nyingine zozote ambazo huhisi ni kosa kuwa nazo.
Nani amekuambia kuwa una kasoro? Mshukuru Mungu kwa kukuumba jinsi ulivyo, amini kuwa Mungu ana makusudi yake kukuumba kama ulivyo.
Kuna watu wengine wanaweza kukupenda kutokana na hizo kasoro unazoziona katika mwili wako!
Kujitoa kasoro na kutojiamini ni kosa kwa kuwa unakuwa unajiathiri kisaikolojia na kujiona hufai kupendwa mwisho wa yote unakuja kumparamia mtu yeyote kwa nia ya kujiondolea mkosi na akishakutumia anakuacha solemba unabaki na machungu moyoni na kujiongezea matatizo zaidi.
Naamini baada ya kujipenda wewe na kujiamini kuwa unavutia, utakuwa katika hali ya kawaida kisaikolojia na wakati mwingine anaweza akajitokeza akupendaye na kukuomba hifadhi ya moyo wake kwako.
Sababu ya kukaa muda mrefu bila mpenzi au kutamkiwa kuwa unapendwa isiwe chanzo cha kupata maumivu mapya ya moyo. Kuachwa kwako, kusiwe chanzo cha kuingia kwa mwingine ambaye anaweza kuwa mwiba zaidi.
Acha papara, tulia, pata wasaa wa kumchunguza huyo anayedai anakupenda kwa muda wa kutosha kwa kuwa inawezekana naye akawa ni mmoja kati ya wale wanaotaka kukufanya chombo cha starehe!
Akikuhitaji kuwa na wewe (huyo mwanaume)lazima umchunguze kwanza na usiruhusu aujue mwili wako kabla ya kuelewa nia yake hasa kwako ni ipi; starehe ya muda mfupi au anakuhitaji kimaisha.
Usifanye mambo kwa papara, unahitaji utulivu wa kutosha ili uweze kumpata yule ambaye ni muhimu kwa ajili yako.
Ukijiamini na kuwa makini ni wazi kuwa utampata yule anayekupenda kwa dhati.

Jenga mazingira ya kuaminiwa ili uwe huru

Kuna mtu aliulizia juu ya tabia ya mpenzi wake kuonyesha hamuamini kwa kila analofanya, akichelewa kupokea simu, akirudi asimkute, akienda dukani akachelewa kidogo, vyote kwake huonekana ni matatizo.
Tabia hizi ni kero pale mpenzi wako anapoonyesha hakuamini kwa kila unalolifanya. Unajiuliza ni kwa nini akuone si muaminifu na bado yupo na wewe?
Hapa kuna kitu cha kuangalia. Pengine huyo mpenzi wako ana wivu wa kupindukia na kuona kila ukiwa peke yako basi akili yako inawaza kusaliti.
Si kweli, si kila mwanamke akiwa peke yake anawaza ngono, kufikiri hivyo ni kosa kubwa na inaonyesha jinsi wanaume wa mfumo huo walivyo na ufinyu wa kufikiria.
Mwanamke anatakiwa kupewa uhuru wa kufanya mambo ya kimaendeleo ambayo wewe mwenyewe unatakiwa kuwa msimamizi.
Wapo wanaokaa nyumbani kwa vile hawana shughuli lakini hawawazi kufanya ngono tu, tabia ya umalaya ni ya mtu wala si kwa sababu ya kubaki peke yake.
Lakini kuna kitu ambacho napenda kukizungumza kwa wapendanao wote hasa wewe mwenye mpenzi mwenye wivu sana. Unapoona huaminiwi basi jenga mazingira ya kuaminiwa ili uwe huru.

Nina maana gani?
Kuna baadhi wa wanawake huwa hawajui wakiwa peke yao waishi vipi na wakiwa ndani ya uhusiano iweje pia. Wengi hujiwekea mazingira hatarishi ambayo kwa mwanaume yeyote rijali, hawezi kuyakalia kimya.
Mfano: Simu unazopigiwa hazieleweki na wakati mwingine ukakwenda kuzungumzia pembeni, kwa nini mwenzako asihoji? Unatoka nyumbani bila ruhusa hata ukiulizwa huna majibu ya kujitosheleza, kwa nini asihoji?
Unakwenda dukani kwa muda mrefu au unasimama na mwanaume na kuzungumza naye vichochoroni, hata kama hamzungumzii mapenzi lakini mpenzio lazima ahoji.

Mazingira ya kuaminiwa
Kwanza, jiheshimu mwenyewe kwa mavazi na muonekano wako, jiepushe na mazoea na wanaume yaliyopitiliza, jiepushe kugeuza simu kama kichaka cha kuficha maovu yako. Mlindie heshima mwenzio hata akiwa mbali nawe.
Punguza vikao na mashoga wasiokuwa wa lazima. Fanya kile anachokitaka mwenzio na kukiacha asichokitaka, kuwa sehemu ya maendeleo yake, onyesha umeolewa kwa kulisema wazi na siyo kuwa msiri ili kujiweka mbali na wanaume wakware.
Ukivifanya vyote hivi vitamfanya mumeo au mpenzio, akuamini hata akiwa mbali na nyumbani.

Mbinu za kumwacha mpenzi wako bila ya kumuumiza

Katika ulimwengu wa mapenzi, kila siku watu wanaingia kwenye uhusiano lakini elewa kwamba siku ambayo wewe unamzimikia mtu flani siku hiyo hiyo wapo wanaozinguana na kuachana.
Si kwa wapenzi tu, hata kwenye ndoa wapo ambao leo hii ndiyo wanaoana lakini leo hii hii kuna wanaopeana talaka. Iko hivyo na kwa maana hiyo suala la kupendana lipo lakini la kuachana nalo halikwepeki.
Ndiyo maana ukijaribu kufuatilia hata wewe unayesoma makala haya yawezekana mpaka umefikia hatua uliyonayo umeshaacha au kuachwa.
Hilo ndilo limenifanya niandike mada hii. Je, unajua mbinu sahihi za kumuacha mtu ambaye mlikuwa mkiambiana I love you, I love you too? Kama jibu ni hapana, leo nitakupa shule inayoweza kukuongoza katika hilo.
Lakini kabla ya kulizungumzia hilo niseme tu kwamba miongoni mwa vitu nisivyovipenda katika maisha yangu ni kusikia flani na flani waliokuwa wanapendana sana hadi kuwa gumzo mtaani wameachana.
Inaniuma kwa sababu najua ivavyouma. Mara nyingi anayeachwa anaumia zaidi hasa akiwa hajajiandaa na ndiyo maana wataalamu wa masuala ya mapenzi wamejaribu kuanisha mbinu ambazo unaweza kuzitumia katika zoezi zima la kumuacha mpenzi au mume/mke wako hasa pale zinapokuwepo sababu za msingi zinazoweza kukubalika.

1. Hakikisha umedhamiria
Unatakiwa uwe umejiandaa kumkosa katika maisha yako. Jadiliana na akili pamoja na moyo wako kama kweli vimeridhika na uamuzi unaotaka kuchukua. Jiulize ni kweli amekukosea kiasi kwamba huwezi kuendelea kuwa naye?

2. Usiwe mwenye hasira
Unapotaka kumuacha mpenzi, mume au mke wako kwa sababu maalum, hakikisha huna hasira.Tulia ili hata pale utakapokuwa hauko naye usije ukajuta na kudhani hukuchukua uamuzi sahihi.

3. Muda na siku sahihi
Wataalamu wa mapenzi wanasema kuwa, muda wa asubuhi siyo mzuri kumuacha mpenzi wako kwani utampa wakati mgumu siku nzima lakini pia kwa wapenzi wanaofanya kazi siku za katikati ya wiki siyo siku nzuri.
Siku ya Ijumaa jioni inapendekezwa kuwa siku nzuri ya kumuacha mpenzi wako kwa maelezo kwamba ataitumia wikiendi kujiliwaza na hata inapofika Jumatatu, anakuwa amepoa tayari kwa kuendelea na majukumu yake.

Kama nilivyosema awali, kila siku watu wanaingia kwenye uhusiano mpya lakini pia wengine wanaachana. Sababu za kuachana kwa wapenzi zinatofautiana ila kikubwa ni kwamba unapoachana na mtu ambaye mlikuwa ‘mwili mmoja’ hutakiwi kumgeuza adui yako kwa asilimia zote, hata kama kakukosea vipi.
Kwa mfano, yawezekana ulitokea kumpenda na kuhisi angeweza kuwa wako wa maisha lakini kadiri siku zinavyokwenda unabaini si mtu sahihi kwako. Katika mazingira hayo suala la kumuacha haliepukiki ila cha kujiuliza ni kwamba utamuachaje?

Je, itakuwa ni sahihi kumuambia laivu kwamba mimi na wewe basi? Inawezekana ukafanya hivyo ila wataalam wa mapenzi hawashauri kwani wanajua madhara ya kutumia mbinu kama hiyo na ndiyo maana wakashauri kutumia njia ambazo zinaweza kusaidia ukamuacha lakini bila kumuumiza na maisha yakaendelea kuwepo.

Jitoe taratibu
Chukulia kwamba umekuwa naye kwa muda mrefu kidogo ukiwa na malengo ya kuingia naye kwenye ndoa lakini katika utafiti wako ukabaini hakufai, unashauriwa kujitoa kwake kimyakimya. Unachotakiwa katika mbinu hii ni kupunguza kumtendea mambo ya kiupendo.
Kwa mfano, unaweza kupunguza kuonana naye, kumpigia simu, kumtumia sms na hata kumsaidia kifedha kama ulikuwa ukifanya hivyo. Kwa kufanya hayo ni lazima ataanza kuona tofauti na kuhisi penzi linaelekea ukingoni.
Aidha, kwa kumfanyia hivyo ni lazima atahoji juu ya mabadiliko hayo. Wewe hutakiwi kutoa maelezo yoyote zaidi ya kuendelea kuyeyusha bila kumwambia wazi kwamba umemtoa moyoni mwako.
Kama huyo mpenzi wako ni mwelewa atagundua kuwa, ndiyo unamuacha kimtindo na yeye ataanza kujiandaa kukukosa, hata pale utakapokata mawasiliano moja kwa moja atakuwa ameshajua kuwa umemuacha hata bila kumueleza.
Ukigundua ameshafahamu kuwa umemuacha, hapo unaweza kumwambia kwa kifupi kwamba umeamua bora kila mmoja aendelee na maisha yake. Kisaikolojia utakuwa hujamuumiza sana lakini tayari utakuwa umemuacha.

Maneno ya busara
Unaweza kumuacha mpenzi wako kwa kutumia lugha ambayo yeye mwenyewe atahisi hukuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima umuache. Mfano: ‘Ashura, kusema ukweli nilikupenda sana na mpaka sasa naamini wewe ni mwanamke wa maisha yangu, sikuamini kama yupo mwanamke mwingine wa kunipa furaha kama wewe lakini kwa hili lililotokea sina jinsi, inabidi nikuache. Utaendelea kuwa rafiki yangu na kama ni kukusaidia nitakusaidia kama rafiki na si mpenzi.”
Hayo ni maneno ambayo mwanaume anamwambia mpenzi wake akimaanisha anamuacha lakini ukiyachunguza utabaini hayachomi sana kwa kuwa anayeachwa bado anapewa nafasi nyingine ya urafiki wa karibu na si mapenzi tena.
Mimi nikushauri tu kwamba, hakikisha unapotaka kuachana na mtu ambaye mmekuwa pamoja kwa muda mrefu unakuwa makini. Hata kama amekukosea vipi lakini busara itumike hasa kwa kuzingatia yale mazuri ambayo aliwahi kukufanyia huko nyuma.

Umempoteza na unataka kumrudisha mikononi mwako

Kugombana ni sehemu ya maisha ya binadamu. Yawezekana kabisa ulikuwa na mwenzi wako ambaye ulimpenda kwa moyo wako wote na sasa mmeachana. Kutengana kuna mambo mengi, wakati mwingine ilikuwa hasira tu.
Siku zote baada ya hasira kuisha, moyo hubaki peke yake katika nafasi yake halisi ya kufanya maamuzi. Hapo ndipo kwenye lengo la mada yetu ya leo. Kwamba kwa msingi huo umegundua kwamba kumbe mpenzi wako uliyeachana naye, bado unampenda.
Kwamba hata makosa aliyokuwa akiyafanya, ulimsababishia au si makubwa kiasi cha kuachana na badala yake mnaweza kukaaa na kuzungumza kiutu uzima na kuyamaliza. Yes! Hilo ndilo ninalotaka kulizungumzia.
Upo tayari rafiki? Je, uko katika kundi hilo? Unataka kumrudisha mpenzi wako wa zamani? Kama majibu ni ndiyo, mada hii inakuhusu sana.

JE, NI SAHIHI?
Baadhi ya watu huamini kwamba kurudi kwa mara nyingine kwa mpenzi wa zamani ni kujidhalilisha, kujishusha na kujisalimisha. Kwamba hakuna mwanaume wala mwanamke mwingine yeyote atakayeweza kuwa naye tofauti na huyo anayemrudia.
Jambo hilo si la kweli hata kidogo, kikubwa cha kuzingatia hapa ni moyo; je, unahisi bado unampenda? Ni kweli naye anakupenda? Kama sifa hizi zipo, hayo mambo madogo ambayo mmetofautiana ni ya kawaida kabisa ambayo mnaweza kurekebishana taratibu.
Kwa msingi huo basi, hakuna tatizo lolote katika kurudiana na mpenzi wako wa zamani, maana tayari unakuwa umeshamjua vya kutosha, hivyo kukupa urahisi wa kufanya yale anayoyapenda na kuepuka asiyopenda jambo litakalozidisha umri wa uhusiano wenu, si ajabu mkaingia kwenye ndoa.

UTAFAIDIKA NA NINI?
Utafiti usio rasmi nilioufanya, unaonesha kwamba zipo faida za kurudiana na mpenzi mliyeachana, lakini kikubwa ni awe moyoni mwako.
Hebu msikie Julius Kihesupe wa Uwanja wa Ndege, jijini Dar es Salaam, ambaye alipata kuzungumza nami hivi karibuni akitoa maoni yake kuhusu suala hili: “Si vibaya kurudiana, maana kwanza mnakomaza uhusiano.
“Kumrudia mtu wako wa zamani maana yake ni kwamba umekubaliana na udhaifu wake wote. Unajua anachopenda na anachochukia, hapo lazima mtadumu. Bila kudanganya, mke wangu wakati wa urafiki wetu, tukiwa na miaka miwili kwenye uhusiano tulitibuana tukaachana.
“Kila mmoja alikaa kivyake kwa miezi kama sita hivi, nikakutana naye Dar, nikiwa nimeachana naye Mbeya, nikamwita tukakaa na kuzungumza, miezi minne mbele yake tukafunga ndoa.”

CHUNGUZA ALIPO
Kitu cha kwanza kabisa ambacho unatakiwa kuchunguza ni mahali anapopatikana kwa wakati huo, nasema hivyo kwa sababu yawezekana alihama makazi, kikazi n.k. Kujua anapopatikana ni mwanzo wa kuelekea kwenye mafanikio ya kumkamata katika himaya yako.

ANA HISTORIA GANI?
Lazima ujue kuhusu historia yake kiuhusiano baada ya kuachana na wewe. Hapo unatakiwa kufanya ‘ushushushu’ wako kimyakimya bila yeye kujua. Ikiwa ameshafanya ‘vurugu’ sana, maana yake ni mtu asiye na msimamo na huenda anaongozwa zaidi na tamaa za kimwili na si mapenzi.
Katika kipengele hiki, ni muhimu sana kujua kama muda huo ambao wewe unahitaji kurudi tena mikononi mwake kama ana uhusiano mwingine. Kimsingi kama atakuwa ndani ya uhusiano, itakubidi uhairishe zoezi lako.
Unatakiwa kufanya hivyo kwa sababu kwanza, anaweza kukubali kuwa na wewe wakati akiwa bado hajaachana na mpenzi aliyenaye kwa muda huo, hivyo kuwa kama mwizi tu kwa mwenzako.
Kubwa zaidi ni kwamba, utakuwa katika mapenzi ya kushea, jambo ambalo si zuri kisaikolojia na hata kiafya.

Kumbuka kwamba, unaweza kuwa na mwenzi wako, mkapendana kwa dhati na mkadumu kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya mkaachana kwa sababu ambazo mnazifahamu wenyewe.
Katika muda mfupi ambao utakuwa umeachana naye, anaweza kufanya mambo ya ajabu sana. Pamoja na kwamba moyo wako unamhitaji, lakini anaweza kuwa tayari ameshapoteza sifa za kuwa na wewe. Katika hali hiyo, ni sahihi kurudiana naye? Bila shaka jibu hapa ni siyo sahihi.
Wiki iliyopita tulianza kuangalia kama ni sahihi kurudi kwa mwenzi huyo, faida utakazopata kwa kurudiana naye, kuchunguza sehemu anayopatikana na kufuatilia historia yake baada ya kutengana kwenu.
Enheee! Sasa twende kwenye vipengele vingine.MAWASILIANO


Ukishachunguza mahali alipo na kuridhika na historia yake ya kimapenzi baada ya kuachana na wewe, sasa unatakiwa kutafuta mawasiliano yake. 
Kupata mawasiliano yake ni hatua ya kwanza, kitakachofuata baada ya hapo ni kujenga mawasiliano. Hapo sasa inategemea na namna mlivyoachana, lakini kama hamkuwa na ugomvi mkubwa sana, basi unaweza kumtumia meseji za kichokozi mara nyingi uwezavyo kwa siku.
Majibu yake ndiyo yatakayokupa mwanga wa kuendelea na kipengele kingine. Kikubwa hapa ni kutozungumzia kabisa mambo ya mapenzi, badala yake iwe ni kumjulia hali na utani wa hapa na pale.MPE MWALIKO


Baada ya kutengeneza mawasiliano naye, sasa unatakiwa kumwalika katika shughuli mbalimbali za kifamilia na binafsi. Mathalani umepata mwaliko wa kwenda kwenye sherehe au hafla fupi ya usiku, omba kampani yake.
Kama mtu mzima atagundua kitu kilichopo moyoni mwako. Hata kama atakuwa mwenye moyo wenye kutu, kutoka naye mbele za watu, kutamfanya akumbuke enzi zenu mlipokuwa mkitoka pamoja, hivyo kufikiria kurudi tena kwako.
Ikiwa ataamua kukuambia kwamba anaona mrudiane litakuwa jambo zuri zaidi, maana atakuwa amekurahisishia, lakini akinyamaza, basi njia inayofuata hapa chini ni muafaka kwake.MVUTE KARIBU YAKO


Sasa unatakiwa kumsogeza karibu zaidi na wewe. Lazima afahamu kwamba, kuna kitu fulani kipo ndani ya moyo wako. Meseji zako zibadilike, kama ulikuwa unamwandikia, “Vp uko poa?” au “Mambo yanaendaje?”, sasa unatakiwa kubadilisha hadi “Niambie sweetie, uko poa?”
Meseji za aina hiyo zitamfanya aone tofauti na inawezekana kabisa akagundua kwamba upo kwenye mawindo ya kumrudisha tena kwako. Katika hatua hii katu hutakiwi kufungua mdomo wako kumwambia kuwa unataka kurudiana naye na badala yake unatakiwa kuacha vitendo vizungumze vyenyewe.OUTING

Kutokana na ukaribu wenu, kumwalika katika mtoko wa chakula cha mchana au usiku, haitakuwa vigumu kwake. Hiyo itakuwa njia nyingine ya kumfanya awe karibu yako zaidi.
Mkiwa katika mtoko huna haja ya kuzungumza chochote kuhusu uhusiano wenu, labda kama yeye ataanzisha mjadala huo. Ongelea mambo mengine ambayo ni maarufu zaidi labda katika duru za siasa, sanaa n.k lakini si mambo yanayohusu mapenzi kabisa.
Kama kichwani mwake alikuwa amekufanya kama rafiki yake wa kawaida, mtazamo utaanza kubadilika taratibu na kuanza kutamani kurudi tena mikononi mwako. Jaribu kufikiria, kama umetoka naye, akiamini labda unataka kumuomba msamaha na kurudiana naye, wewe unaanza stori za soka! 
Bila shaka atajiona kama mpumbavu kichwani, si ajabu akaamua kujifunga mwenyewe kwa kuomba urudi tena kwake.

JADILI PENZI LENU


Hatua hii ndiyo muhimu zaidi hapa; sasa unatakiwa kuanza kuzungumzia juu ya uhusiano wenu. Mwambie jinsi ulivyokuwa ukifurahishwa na mapenzi yenu. Msifie alivyokuwa anajua majukumu yake na kukuonesha mapenzi ya dhati.
Si vibaya kama utamweleza pia sababu ambazo unahisi zilisababisha wewe na yeye kuachana. Kwa kauli hizo utampa nafasi ya kuchambua/kumjua mwenye makosa na mahali pa kurekebisha.KIRI MAKOSA YAKO


kiwa kuna mahali unaamini ulikwenda kinyume na yamkini ndiyo sababu kuu iliyosababisha muachane, kiri makosa yako mbele yake. Mweleze kwamba wewe ndiyo chanzo cha matatizo na huenda kama si kukosea, msingeachana.
Kujutia hasa kama uso wako utawakilisha vyema kilicho moyoni mwako, kutamfanya akuone muungwana ambaye unatambua ulipojikwaa na sasa unataka kurekebisha makosa yako. Hapo utakuwa na nafasi kubwa ya kumnasa kwa mara nyingine.MWELEZE YAKO YA MOYONI


Sasa huna sababu ya kuendelea kujitesa, toa dukuduku lako. Mwambie moja kwa moja kilichopo moyoni mwako. Kwamba unahitaji nafasi nyingine kwake, maana umeshajua makosa yako.
Hii ni nafasi ambayo si rahisi kabisa kuchomoka. Itumie vilivyo. Sauti yako pekee itoshe kumaanisha kile kilichopo moyoni mwako. Lazima atakuelewa.
Kama utakuwa umefuata kwa makini vipengele vyote hapo juu, lazima urudi tena mikononi mwake. Kuna nini tena? Ameshakuwa wako huyo, ila kuwa makini usimpoteze tena.

AKIKATAA JE?
Pamoja na kufuata vipengele vyote hivyo, inawezekana akakataa. Kukataa kwake lazima kuna sababu nyingi. Mwingine anaweza kukuambia moja kwa moja sababu za kukataa kurudiana na wewe wakati mwingine anaweza asiseme chochote.
Huenda akakumbia kwamba tayari ana mtu wake, au hafikirii kurudi mikononi mwako; usihuzunike.
Ni bora sana huyu anayekuambia ukweli, kuliko kurudi halafu ukutane na mateso yale yale.Inawezekana labda hana mapenzi na wewe. Kama ndivyo, kuna sababu gani ya kujikomba? Kubaliana na ukweli, halafu subiri mwingine!
Sikia, subiri mwingine na siyo utafute, maana mwenzi wa kweli huja mwenyewe, hatafutwi!